ABIRIA WA NDEGE MJINI BUKOBA WAKWEA BUS KUFUATIA RATIBA KUTOKUELEWEKA
Habari zisizo RASMI zinasema kutokueleweka kwa ratiba za NDEGE mjini hapa ni kutokana na ukarabati na upanuzi wa uwanja huu wa ndege kwa kiwango cha lami, hivyo uwenda ukafungwa kutumika kwa muda.
Camera yetu ikiangaza kipande chenye lami, uku mvua ikiendelea kunyesha na kufanya wahusika wapate sababu ya hali ya hewa ingawa tatizo la ratiba limejirudia kwa siku ya pili pasipo mvua kunyesha wala wingu kutanda!!
Baadhi ya abiria wanaoelekea jijini Mwanza kwa ndege ya shirika la ndege la Precision Air wakiwa katika sintofahamu baada ya kushindwa kusafiri kwa siku ya jana kwa mujibu wa ratiba ilivyokua na pasipo kupewa ujumbe wowote kama inavyoeleweka ,kwa dhana wangesafiri badae ama siku inayofuata.
Uku wakiwa wamepoteza mwelekeo na kuwaladhimu wengine kukodi magari binafsi na wengine kukwea bus lililofika uwanjani hapo.
Mdau Ibra ambaye ndiye dereva wa bus la Minziro kwetu linaloelekea Mwanza kwa kila siku akiwa katika utayari wa kuanzisha safari.
Muonekano wa kipande cha lami katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa ya Bukoba.