CHADEMA inasimama na Lwakatare, maamuzi ya Kamati Kuu
Jana akitoa briefing ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA mbele ya
wanahabari (nakala ya kilichozungumzwa iko hapa JF), Mkurugenzi wa
Katiba na Sheria wa CHADEMA, Tundu Lissu aliweka wazi moja ya masuala
ambayo watu wengi wamekuwa wakihoji, wakiwemo waandishi wa habari, kwa
nini CHADEMA inasimama na Lwakatare!
Lissu alisema, azimio la kikao cha Kamati Kuu na hivyo msimamo wa CHADEMA ni kwamba chama kitasimama na kumtetea Lwakatare kwa gharama zote, ikiwemo kumwekea utetezi wa kisheria kwa sababu kesi hiyo ya ugaidi ni kesi ya uongo, kesi ya kutungwa na watawala (CCM) kutafuta namna ya kuondokana na 'headaches' za CHADEMA.
Alisema wazi kuwa CHADEMA isipoweza kumtetea Lwakatare, haitaweza kumtetea mtu mwingine yeyote yule dhidi ya tuhuma za namna hii, ambazo zimeandaliwa na zinaandaliwa nyingi. Kamati Kuu iliona kufanya hivyo ni kujitumbukiza kwenye mtego wa CCM ambao wangependa kuona hilo linatimia.
Kesho watamtengenezea tuhuma na kumshtaki Naibu Katibu Mkuu, kesho watamuundia tuhuma Katibu Mkuu, keshokutwa wataunga unga maneno kumtungia mashtaka Mwenyekiti wa chama, leo itakuwa kwa mkurugenzi, kesho huyu keshokutwa yule. Mtawatosa wote. Ndivyo wanavyotaka. Kisha wataenda hatua nyingine wanayokusudia katika adhima iliyoshindwa mapema, ya kuimaliza CHADEMA, tumaini jipya la watu.
Kwa mujibu wa Lissu, Kamati Kuu ilifikia uamuzi huo baada ya kupewa taarifa ya kina juu ya makando kando mengi kuhusu suala la Lwakatare kubambikiwa kesi ya ugaidi.
Ni makando kando hayo yaliyowasilishwa mbele ya Kamati Kuu kwa ushahidi wa kina, yanakiweka na kuonesha wazi namna CCM ilivyo katikati ya mchezo mzima, kwa asilimia karibu zote kupika tuhuma na kisha kesi hiyo kwa kusudio la kutaka kuonesha kuwa viongozi wa CHADEMA na hatimaye chama hicho kinajihusisha na masuala ya ugaidi na mipango ya mauaji ya raia. Lengo; bambika tuhuma, label CHADEMA, tafuta visingizio vya msajili kufuta CHADEMA, kosanisha na wanahabari.
Kwa mujibu wa Lissu, unawezaje kumtosa Lwakatare katika kesi ambayo involvement ya CCM na watu wengine fulani fulani katika kutengeneza suala hilo ni kubwa kwa kiwango kisichotiliwa shaka kuwa mchezo huu umetengenezwa! Unawezaje kumtosa kamanda wako katika suala ambalo CCM na watawala, kupitia vyombo vya dola, wanakesha wakipanga mipango ya ku-fubricate (that is criminal) ushahidi kumhusisha Lwakatare, viongozi wengine na chama katika matukio ya kutunga?
Lissu alihoji juu ya mawasiliano makubwa hadi ya kutumiana pesa kati ya mtu aitwaye Mwigulu Nchemba na Ludovick Lwezaura, hadi kutumiana fedha kwa njia ya Mpesa, siku chache tu baada ya video hiyo kutengenezwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba kuwa ameitangazia dunia kupitia Star tv kuwa anao mkanda/CD inayoonesha viongozi wa CHADEMA wakipanga njama za mauaji. Je, Mwiguku alikuwa na biashara gani na mtuhumiwa wa ugaidi, Ludovick?
Hiyo ni mbali na yale mawasiliano yaliyofanyika kati ya Ludovick na Mwigulu siku ile ile ambayo video inaonekana ilichukuliwa. Wana uhusiano gani, Kiongozi mwandamizi wa CCM na mtuhumiwa wa ugaidi!
Mwanasheria msomi Lissu, mmoja wa mawakili wanaomtetea Lwakatare, alisema kumekuwepo na mawasiliano ya kiwango cha juu kati ya mtu aitwaye Ludovick Joseph Lwezaura na Dennis Msaki. Alihoji iweje Msaki awasiliane mara nyingi zaidi na mtu anayetuhumiwa kutakiwa kumlisha Lissu au kumteka, kuliko hata alivyoweza kuwasiliana na mke wake!
Kwa mujibu wa Lissu, Kamati Kuu pia ilipokea taarifa namna watu wanaodaiwa kuwa ni watumishi wa vyombo vya dola, wanamtumia mtu aliyewahi kufanya kazi Makao Makuu ya CHADEMA (kabla hajafukuzwa mwanzoni mwa mwaka jana kwa tuhuma za ukosefu wa uadilifu), kwanza kuwarubuni watumishi wa idara fulani waibe nyaraka za CHADEMA kwa ahadi ya fedha nyingi.
Pili, kuwarubuni watumishi wa CHADEMA Makao Makuu wanaohusika na ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake, wakubali kuandika maelezo ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi ya Lwakatare, viongozi wengine na chama kwa ujumla, mahalamani.
Walinzi hao wa CHADEMA wameshaitwa katika vikao mara tatu sasa, mojawapo ya maeneo ya makutano ikiwa ni Sea Cliff Hotel na Jakees. Wanafundishwa namna ya kuandika maelezo, huku wakiambiwa wawe tayari kushikiliwa kwa muda polisi, lakini baadae wataishi maisha mazuri (huko waliko) kwa kupewa pesa na familia zao zitawezeshwa kwa muda wote. Yote ni katika kutengeneza ushahidi. Lissu alisisitiza kuwa kutengeneza ushahidi ni kosa kisheria. Ni kosa hata liwe limefanywa na nani!
Pia wameombwa wawe tayari kutoa maelezo ya uongo kwenye vyombo vya habari, ili kukichafua chama, kukipaka matope meusi ya kuwa ni chama cha kigaidi kinahusika kupanga njama za mauaji. Yote hii ni mwendelezo wa siasa chafu za maji ya mtaroni. Gutter politics. Ambazo, kwa mujibu wa Lissu mbele ya wanahabari, zilianza na kuita CHADEMA 'chama cha familia ya Mtei na Mbowe, chama cha Wachaga, chama kikabila, chama cha Kaskazini, chama cha Wakristo, chama cha Wakatoliki...aah aah chama cha Wakatoliki' yote hayo yameshindikana. Sasa ni zamu ya 'chama cha ugaidi, chama cha mauaji'.
Makando kando ni mengi. Kila jambo na wakati wake. Ni muhimu kuwa na akiba ya maneno. Lissu alisema yako mengi yatasemwa wakati mwafaka ukifika.
Lissu alimalizia kwa kuwapatia mfano waandishi wa habari, namna ambavyo TANU ilikuwa tayari kumlinda kwa gharama yoyote Mwalimu Nyerere pale wakoloni wa Kiingereza walipombambikia tuhuma na kumfungulia kesi ya uchochezi na wenzake wawili, wanahabari wenzetu Robert Makange na Rashid Bagidele. Ilikuwa mwaka 1958.
TANU iliweka mawakili watatu, kutoka Uingereza, mwingine Kenya na mmoja akiwa Mtanzania. Kumtetea 'mcochezi' Nyerere, ambaye wakoloni walitaka kumpeleka gerezani, kwa kuonesha kuwa ni kiongozi mchochezi, na hivyo TANU kilikuwa chama cha wachochezi, wanaochonganisha wananchi na serikali, wanaotaka wananchi waichukie serikali yao, hivyo ni chama kisichofaa. Kifutwe. Ilishindikana kwa sababu TANU, na Watanzania walisimama na kiongozi wao, wakiamini hakufanya hivyo.
Lissu alitumia mifano kadhaa.
Upo pia mfano mwingine wa Nelson Mandela. Huyu makaburu walisema ni gaidi. Wakamkamata na kumweka gerezani. Kumbukumbu zinaonesha, CIA wamemwondoa Mandela katika orodha yao ya magaidi duniani, mwaka 2007 hivi.
Hivyo ANC walipaswa kumtosa Mandela baada ya kutungiwa tuhuma na kubambikiwa kesi na makaburu, ambao walikuwa wanaona dawa pekee ya kuzuia mapambano ya kumkomboa mnyonge Afrika Kusini kwa kuuondoa utawala dhalimu wa makaburu (hapa kwetu ni CCM, maana kaburu si rangi) ni kudhibiti na kufungia/ kufuta ANC kwa kuanza na viongozi wake?
Hivyo Kamati Kuu ya CHADEMA, ambayo ni chombo cha juu cha maamuzi ya chama, ikaweka azimio la kuwatetea makamanda wake wanaobambikiwa tuhuma za uongo, ambapo lengo kuu la 'wabambikaji' ni kutafuta sababu ya kutesa/kukatisha tamaa wanachama na viongozi (kuweka mahabusu au gerezani) kukichafua chama na hatimaye kutafuta sababu ya kukifuta.
Lissu alimalizia kwa kusema "wanapambana na wazo ambalo muda wake umeshafika. Halizuiliki. Hawataweza. Tutawashinda"
Makene
0752 691569/0688 595831