Bukobawadau

MKUU WA MKOA WA KAGERA NA WAANDISHI WA HABARI WAJADILI MAANDALIZI YA SIKU YA MASHUJAA KITAIFA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabiani Massawe akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari .kuhusu umuhimu wa maadhimisho hayo Mkoani Kagera na kuwataka waandishi kuwahamasisha wananchi kupitia vyombo vya habari na kutumia nafasi hiyo kutangaza fursa mbalimbali zilizopo Mkoani Kagera.Pembeni mwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Nassoro Mnambila akinukuu mambo muhimu wakati wa kikao hicho.
 .Waandishi wa habari Antidius Kalunde(Tanzania Daima na Method Kalikila Rumuli)wakifuatilia majadiliano
Mjumbe wa Bodi ya Redio Karagwe(Clement Nshelenguzi)na Mwandishi kutoka Radio Fadeco ya Karagwe wakifuatilia majadiliano katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Mkurugenzi wa Radio Fadeco Joseph Sekiku na Mkurugenzi wa Redio Kasibante wakijadiliana jambo wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa na Waandishi wa habari wakati wa kuweka mikakati ya kufanikisha Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Kitaifa ambayo mwaka huu yatafanyika Kitaifa Mkoani Kagera  tarehe 25,Julai katika Kambi ya Kaboya
Maofisa kutoka Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa nao walikuwepo wakati wa kikao hicho cha maandalizi ya Siku ya Mashujaa Kitaifa,ambapo hii itakuwa mara ya Pili Mkoa wa Kagera kupewa heshima hiyo,baada ya maadhimisho kama hayo kufanyika mwaka 2009.
Ofisa Utamaduni wa Mkoa wa Kagera Kepha Elias na Ofisa Habari wa Mkoa Silvestery Raphael wakifuatilia matukio muhimu wakati wa kikao hicho.
Mwandishi wa TBC Charles Mwebeya na Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Audax Mutiganzi(kulia)wakifuatilia hoja za wachangiaji wakati huo Audax akipekua taarifa mbalimbali kwenye mtandao.
Badhi ya waandishi waliohudhuria kikao hicho wakifuatilia kwa umakini.
Picha kwa hisani ya Phinias Bashaya
Next Post Previous Post
Bukobawadau