Bukobawadau

BALOZI KAGASHEKI AMKINGIA KIFUA KINANA

 Kuhusu tuhuma kwamba  Kinana alikuwa anajihusisha na masuala ya kusafirisha meno ya tembo baada ya meli iliyofanyiwa kazi na Kampuni ya Sharaf kukamatwa nchini China ikisafirisha meno hayo.
Kagasheki alisema ni makosa kwa Kinana kutuhumiwa wakati kilichokuwa kimebebwa kwenye meli hiyo hakikuwa mali yake.

“Hivi ina maana wamiliki wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) au wale wa Precission Air ndiyo wanapaswa kutuhumiwa kwa kile kinachobebwa na abiria wao kweli?

Ndugu yangu Mchungaji Msigwa anafahamu ninamheshimu sana. Ingawa amenirushia makombora mengi sana. Lakini katika hili nadhani hata kama ni siasa nadhani ni kitu ambacho hakikubaliki kwa wastaarabu,” alisema.

Hata hivyo, Balozi Kagasheki aliahidi kuwa Serikali imepanga kufanya operesheni dhidi ya majangili wa meno ya tembo.
Alisema hawatatangaza siku ya operesheni hiyo kutokana na kuwahusisha watu wengi.

Loliondo
Kuhusu mgogoro wa siku nyingi wa Loliondo, Balozi Kagasheki aliahidi kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atatolea ufafanuzi suala la eneo tengefu la Loliondo wakati wowote katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti.

Alisema Serikali imeshughulikia kwa nia njema suala hilo lakini kutokana na malalamiko ya wananchi kufikishwa kwa Waziri Mkuu, wanasubiri uamuzi wake.

Loliondo kuna mvutano mkubwa kutokana na wananchi kupinga mpango wa Serikali kutwaa hekta 1,500 za mraba kutoka katika ardhi ya vijiji kama eneo tengefu.
Source;Mwananchi
Next Post Previous Post
Bukobawadau