Bukobawadau

BREAKING NEWS!! RUAHA KIMENUKA, RAIA WAPIGWA MABOMU!

Habari zilizopo hivi sasa kutoka Ruaha wilaya ya Kilosa mkoani Moro ni kwamba kuna mapambano yanaendelea hivi sasa kati ya raia na askari wa kutuliza ghasia ambao wanatawanya raia kwa mabomu ya machozi. Imeelezwa na ripota wetu kutoka Ruaha kuwa chanzo cha mapambano hayo ni mvutano ulioibuka kati ya Wanakijiji na Serikali ya kijiji cha Ruaha, baada ya wanakikiji kuutaka uongozi uachie ngazi na uongozi kugoma kuachia ngazi. Imeelezwa zaidi kuwa kufuatia hali hiyo, wanakijiji walivamia ofisi za serikali ya kijiji na kukiteka hali iliyowalazimu askari kuitwa ili kutawanya raia.
Hali haikuwa rahisi, kwani raia waligoma kutawanyika na askari wakalazimika kufyatua mabomu ya machozi ambayo yalipigwa mpaka yakaisha lakini raia wakawa bado wapo, askari walilazimika kufuata mengine na hali bado ni tete hadi muda huu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau