Bukobawadau

MUENDELEZO WA MATUKIO KUHUSU MTWARA

 Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)

 Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao. Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
 RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.(chanzo Jamii Forums)

Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.

Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.

Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote

Barabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita.
Next Post Previous Post
Bukobawadau