PICHA ZA ZA TUKIO ZIMA LA KULIPUKA KWA BOMU KANISANI ARUSHA LEO!!!
Inasemekana mtu mmoja amefariki kwenye mripuko wa bomu kama saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha, Tanzania.
Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mara tu baada ya tukio hilo
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
Wengine kadhaa walijeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya kuzindua parokia mpya ya mtakatifu Yosefu walinusurika.
Kwa mujibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha, mripuko ulipotokea walikuwa tayari kubariki maji kwa ajili ya uzinduzi wa kanisa, shughuli iliyokuwa ikiongozwa na balozi wa Papa Francis.
Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali, kuna watu watatu kati yao waliofariki na wengine wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru mjini Arusha
Watalaalamu wa miripuko na polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.
Bado hakuna taarifa ya chanzo cha mripuko au kama kuna mtu au kundi lilohusika.
Hili ni shambaulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japokuwa mwaka huu pia kulikuwa na tukio la mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar, ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia kanisani.
Polisi waki imarisha doria eneo la tukio baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu zaidi
Sehemu mripuko ulipotokea.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.