Bukobawadau

Taswira Clouds Media Group ikizindua msimu wake mpya Jana Mjini Dodoma.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa Muziki hapa chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini hiyo iliyohusu na  harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa Dodoma.kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa.  Aidha pia mchana huu kutakuwepo na burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania katika uwanja wa jamhuri .
Pichani ni washiriki wa semina hiyo kutoka sehemu mbalimbali mjini Dodoma leo.
 Mh Zitto kabwe akimsikiliza mmoja wa washiriki wa semina hiyo alipokuwa akiulizwa kuhusiana na suala la fursa zinazopatikana kwa vijana na namna ya kuzitumia katika ujumla wa kujikwamua na ugumu maisha,ambapo watanzania wengi wamekuwa wakizilalamikia
 Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Zenno  Ngowi kutoka kampuni ya Tanzania Home Expo akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ardhi,ujenzi,na mengineyo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria kwenye semina hiyo  mjini Dodoma.
 Mmoja wa wasanii mahiri wa Mashairi,Mrisho Mpoto akifafanua jambo kuhusiana na mambo mbalimbali katika suala zima la wasanii kujipa nafasi ya Fursa mbalimbali zinazojitokeza mbele yao na namna ya kuzifanyia kazi na kuziboresha zaidi.


Mtangazaji wa Clouds FM,Loveness Love a.k.a Diva akijitambulisha kwenye semina hiyo
Mtangazaji wa Clouds FM,Shaffih Dauda akijitambulisha kwenye semina hiyo.
wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo iliyoibua changamoto nyingi.
Kutoka Clouds FM,Millard Ayo,Dina Marios pamoja na Zamarad wakifuatilia jambo
Mtangazaji wa Clouds FM,Arnold Kayanda  akijitambulisha mbele ya washiriki waliofika kwenye semina hiyo.
Baadhi ya wasanii wakiwa ndani ya semina hiyo katika harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi zao,ambapo matembezi ya hisani yamepangwa kufanyika kesho na Waziri Mkuu Mh.Pinda anatarajiwa kuyapokea matembezi hayo.
Msanii Afande Sele na Msanii mwenzake wakiwa ndani ya semina hiyo wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa.
Mtangazaji wa Kipindi cha jahazi,Mussa Hussein akijitambulisha.
Mtangazaji wa Clouds FM,B Dozen akijitambulisha
 Mbwiga Mbwiguke nae kama kawa akijitambulisha kwa washiriki wa semina hiyo.
Zamarad Mketena akijitambulisha pia.

 Wakazi wa Dodoma walivyo pokea kwa kishindo msimu mpya wa Clouds.
 Mikono ya Dj inahusika katika kuwapagawisha watu

Picha kwa hisani ya Teentz.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau