Bukobawadau

GHARAMA ZA SIMU KUPANDA MWEZI UJAO

Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma hizo zinatajiwa pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka huu.Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazotoweza kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.MOAT inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zinaendelea kutoza viwango vya ushuru kwa asilimia 10 na 12.5.
Next Post Previous Post
Bukobawadau