Bukobawadau

HABARI MBALIMBALI KWA MKUTASARI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza askofu Telesphori Mkude wa jimbo katoliki Morogoro wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya Uaskofu wake (Silver Jubilee)zilizofanyika katika viwanja vya St.Peters junior Seminary mjini Morogoro leo
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu Katoliki wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 25(Silver jubilee) ya Uaskofu wa Askofu Telesphori Mkude wa jimbo Katoliki Morogoro zilizofanyika katika Viwanja vya Seminary ya St.Peters mjini Morogoro leo.(picha na Freddy Maro) 
Mwigulu Nchemba Nusura Amchape Peter Msigwa
Dodoma, Tanzania. Katika tukio lililotokea leo kwenye ukumbi wa St.Gasper Dodoma ambako wabunge wote wapo kwenye semina ya masuala ya ukimwi ambayo inaendelea kumetokea mtifuano na nusura Mwigulu arushe ngumi baada ya Mch.Msigwa kumuita kuwa ni muuaji na hivyo atubu kutokana na damu za watoto wadogo na wakina mama wa Arusha ambao amekatiza maisha yao kwa sababu ya ukatili ambao hauwezi kuendelea kuvumiliwa kamwe.

Tukio hili lilifuatia baada ya wabunge wa Chadema ambao wameanza kurejea Dodoma kwenye Semina hiyo walipokuwa wakiwaambia wabunge wa CCM kuwa Bunge linarejea jumatatu kwani sasa limeshamaliza kukaaa kama kamati ya matumizi , hivyo litarejea kwani wabunge wa Chadema watakuwepo hali iliyozidisha hasira za wabunge hao ambao wengi wanaonekana kuwa na hang over za jana ktk kumuaga Sitta.

Mwigulu alinyanyuka kwenye kiti na kumfuata Msigwa na kumshika kifuani ila wabunge wenzake walienda kuamulia ugomvi huo na hali bado iko tete, semina inaendelea


Kijana Edward J. Snowden (pichani), mfanyakazi wa zamani wa wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani (NSA) aliyevujisha nyaraka nyeti zinazohusu mawasiliano ya watu yanayonaswa na wakala hiyo kwa vyombo vya habari amefunguliwa mashitaka ya kuvunja sheria ya Ujasusi na kuiba mali ya serikali ili kuvujisha taarifa nyeti kwa gazeti la Guardian na Washington Post, Idara ya Sheria ya nchi hiyo imesema.Kila kosa katika hayo matatu aliyoshtakiwa nayo yanabeba adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela, na habari zinasema huenda akaongezewa mashtaka
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo ambaye pia ni mjumbe wa NEC Dkt Fenella Mukangara akibidhi vifaa vya michezo kwa Katibu wa UWT kata ya Ubungo Bi. Rose Ndunguru.Vifaa hivyo vimetokana na ombi maalum kwa ajili ya ligi ya mpira wa Pete inayojulikana kama Rose Wasiri Cup.Mashindano hayo yameanza leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vilivyoko Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam.Jumla ya mipira tisa na seti mbili za jezi zimekabidhiwa


Hiki ndicho alichokiandika Mbunge wa Mbeya Mjinikatika ukurasa wake wa Facebook, Sugu ameandika “…Tanzania haijawahi kuwa na waziri mkuu mpumbavu kama mizengo pinda…alichokifanya ni kutangaza rasmi vita kati ya serikali ya ccm na raia wa tanzania…!!
Kauli ya Sugu imefuatia kauli ya waziri mkuu Mizengo Pinda kuwaruhusu rasmi polisi kutumia nguvu ya ziada kuwadhibiti na kuwapa kichapo wafanya fujo.
Spika wa Bunge Mstaafu,Mh. Samuel Sitta aagwa rasmi mjini Dodoma
Picha ya Meza kuu wakati wa hafla hiyo Spika wa bunge Anne Makinda akizungumza katika hafla ya kumuaga Spika Mstaafu Samuel Sitta kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma juni 21, 2013. 
Next Post Previous Post
Bukobawadau