Bukobawadau

MAMBO SASA SI MAMBO CHADEMA BUKOBA,LWAKATARE NITAPAMBANA NA WANAOTAKA KUNIPINDUA

Ni baada ya mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho kuhutubia mkutano wake wa kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana, ambapo amehutubia wana Bk kupitia uwanja wa uhuru Mayunga mjini Bukoba.

Katika mkutano huo, Ndg Lwakatare ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Kagera, amekuta viongozi wa chama hicho mkoani hapo wakifanya njama za kumpindua kwa kufanya mipango ambayo hakuitaja lakini akasema amepata taarifa za mkutano wao uliofanyika wilayani Muleba.

Amesema walikuwa wakifurahi kusikia ananyimwa dhamana wakiomba aendelee kushikiliwa na waliposikia kaachiwa walipanga mikutano ya haraka kuweka mambo yao sawa.B wana Lwakatare anasema kuwa kwa mara ya kwanza amemwomba Mungu siyo kama alivyokuwa akimbip wakati huo, kwakusema kuwa alitoka CUF akidhani anakimbilia CHADEMA kutakuwa hakuna wanafiki kama alikotoka lakini kumbe huku CHADEMA ndiyo balaa. Amesisitiza kuwa kwakuwa yeye ni mkurugenzi wa usalama wa chama taifa lazima atapambana na wanafiki ndani ya chama

Ametoa mfano kuwa ni bora akapambana na Mwigulu Nchemba, na akina Kagasheki ambao anajua kuwa wanapambana kwa hoja za vyama vayo kuliko kupambana na wanafiki ndani ya chama cha CHADEMA na kuomba msaada wa kuendesha mikutano ya kata kabla hajarudishwa ndani
Next Post Previous Post
Bukobawadau