Bukobawadau

Soseji za minofu ya samaki katika maonyesho ya Saba Saba Dar

 Soseji za monofu ya samaki ambazo ziko tayari kwa matumizi
Mjasiliamali Mery Kalega ambaye ndiye mbunifu wa bidhaa hiyo hasa kwa wale wasiopenda matumizi ya nyama.

WAJASILIAMALI wameanza kuibuka na mbinu mpya za kuongeza thamani ya mazao baada ya minofu ya samaki kuanza kutumika kuzalisha bidhaa mpya ambayo kabla haikuwahi kuonekana sokoni.


Ubunifu huo umeibuliwa na mjasiliamali Mery Kalega ambaye kwa kutumia minofu ya samaki ameweza kutengeneza soseji na ubunifu wake anatarajia kuupeleka kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa yatakayoaanza wiki hii jijini Dar es salaam.

 Kwa mujibu wa mjasiliamali huyo anayeendesha shughuli zake nje kidogo ya mji wa Bukoba alisema bidhaa hiyo mpya inawafaa watumiaji wa aina zote hasa wale wasiopenda soseji za  nyama ambazo kwa kiasi kikubwa ndizo zimezoeleka kwenye soko.

Alisema bidhaa hiyo aliianza kwa majaribio kwa kutumia minofu ya samaki kutoka kiwandani na kuwa ni mzalishaji wa kwanza wa bidhaa hiyo na kuwa pamoja na kuwa ni bidhaa ngeni sokoni tayari imepata watumiaji wengi.

‘’Huu ni ubunifu wangu wa kuongeza thamani ya mazao ya samaki,mimi ni mzalishaji wa kwanza wa soseji zinazotokana na minofu ya samaki pamoja na kuwa bidhaa hii haijafahamika sana’’alisema Kalega
Pia alisema anafanya jitihada za kujiimarisha katika soko la ndani na moja ya mipango hiyo ni kushiriki maonyesho ya Kimataifa ya biashara katika banda la Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo Sido ambayo yatafanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni.
 Aidha alisema wajasiliamali wanatakiwa kuondoa uoga katika biashara na kuwa wanatakiwa kuwa wabunifu kwa kuangalia mahitaji ya soko huku wakiboresha thamani ya mazao yao.Mjasiliamali huyo anapatikana kwa simu namba 0754759055.


 Mery Kalega akiwa ofisini kwake nje kidogo ya mji wa Bukoba

Ukaangaji wa soseji za samaki
Next Post Previous Post
Bukobawadau