Bukobawadau

TASWIRA MAZISHI YA ALBERT MANGWEA

Hapa watu wanakanyagana kwa ajili ya kujipanga mstari kwenda kumuaga marehemu Ngwair, leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ulikuwa umejaa watu, sambamba na wale waliojipanga barabarani kwa ajili ya kuangalia msafara wa Ngwair uliofunika mji wote siku ya leo.

Tukio la kuzikwa lilitanguliwa na shughuli ya uagaji iliyofanyika pia katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, baada ya kuona mkanyagano wa watu wengi nyumbani, usiku wa Jumatano, ambapo taarifa za kuwasili kwa mwili wa Ngwair zilienea.
 Mbunge Mr 2 AKA Sugu anamuaga Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

 Hapa M to The P akilia baada ya kupita kwenye jeneza la Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Kihonda Kanisani jioni yake.
 Taswira Maelfu ya wakazi wa Morogoro wakiwa katika foleni kumuaga marehem Albert Mangwea Safari ya mwisho ya Mareemu Mangwea.

 Mama wa Ngwair akizungumza na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Bendera, leo mjini Morogoro, kabla ya mazishi ya msanii huyo wa Hip Hop Tanzania
Wema akiwa msibani morogoro
 R.I.P MANGWEA.
Next Post Previous Post
Bukobawadau