Bukobawadau

M23 waweka picha ya passport ya “askari wa Tanzania” waliyemkamata akishirikiana na FDLR

Waasi wa M23 wa DR Congo, wanadai kuwa wamemkamata askari wa Tanzania anayeitwa Christopher George Yohana, wakati akishirikiana na waasi wa Rwanda (FDLR) wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya Watusi mwaka 1994
M23 waweka picha ya passport ya “askari wa Tanzania” waliyemkamata akishirikiana na FDLR
Waasi hao wa M23 wameweka picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. Kwa mujibu wa chimpreports.com, M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47 yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook ikiambatana na picha hiyo:

“leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe. Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”
Next Post Previous Post
Bukobawadau