Bukobawadau

MIRADI 78 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI KUMI NA MOJA ILIZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU MKOANI KAGERA 2013

Hapa Baada ya Mwenge wa Uhuru Kumaliza Mbio zake Mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa wa Kagera Anaukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa Kigoma Hiyo Ilikuwa Julai 9, 2013.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian Massawe Akipokea Mwenge wa Uhuru Kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Said Magalula Tarehe 01/07/2013 Mwenge Ulipoingia Mkoani Kagera
 Jengo la Hospitali ya  Manispaa ya Bukoba  Iliyowekewa Jiwe la Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2013 Ndugu Juma Ali Simai. Hospitali inajengwa Katika Eneo la Kyabitembe Manispaa ya Bukoba
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2013 Ndugu Juma Ali Simai Akizindua Rasmi Jengo Hilo.
Vikundi vya Akina Mama Wilayani Kyerwa Vikipewa Hundi ya Mikopo Nafuu Sana Kuendelea Kujiajili Vyenyewe


 Hizo ni Mbwembwe za Mwenge Mkoani Kagera, Wasukuma ni balaa unajionea mwenyewe Mbwa kabebwa mgongoni na katulia tuli na kushikilia.
 Wananchi wa Mkoa wa Kagera Wakiwa juu ya Mti bila kujali kuwa wanahatarisha Maisha yao lakini hiyo yote ni kutaka kuuona Mwenge wa Uhuru na Waliuona na Kufariji Nyoyo zao
Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2013 Ndugu Juma Ali Simai Baada ya Kuzindua Mradi wa Maji Wilayani MIssenyi Anamtwisha Mama Kuonesha Kuwa Mradi Huo Unatoa Maji Kweli
   
Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikimbizwa mkoani Kagera kuanzia tarehe 1-8/07/2013 na kukagua, kuweka mawe ya msingi, kufungua pia  kutoa mikopo kwenye miradi 78 yenye thamani ya shilingi 11,532,867,205.
Miradi hiyo ni pamoja na ya Elimu 13, Afya 13, Maji 6, Kilimo 10, Barabara 2, Hifadhi ya Mazingira 8. Pia Mwenge wa Uhuru ulizindua miradi ya jamii 26 ya vikundi vya vijana, akina mama na  Klabu za wapinga rushwa shuleni, na kukamilisha jumla ya miradi 78.
Kati ya miradi 78, miradi 24 ilizinduliwa, 15 ilikaguliwa, 28 iliwekewa mawe ya msingi, 8 ilifunguliwa, na miradi 3 ilipatiwa mikopo ili kuwawezesha vijana na akina mama walijiunga kwenye vikundi kujiajili wenyewe na kupunguza tatizo la ajira mkoani Kagera.
Miradi hiyo 78 iliyozinduliwa, kukaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kufunguliwa  na Mwenge wa Uhuru Mkoani Kagera imegharimiwa na serikali kuu kwa shilingi 3,074,556,409 Halmashauri za Wilaya shilingi 515,277,176 Wahisani shilingi 2,530,553,348 Jamii shilingi 5,412,480,272 na kukamilisha jumla shilingi bilioni 11,532,867,205.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe alipokea  Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Said Magalula Julai 1, 2013 na kuukabidhi Mwenge huo katika mkoa wa Kigoma Julai 9, 2013 baada ya kumaliza mbio zake mkoani Kagera.
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013 zinaongozwa na Ndugu Juma Ali Simai Kutoka Kusini Unguja akishirikia na wenzake watano wanaoukimbiza Mwenge huo kitaifa ambao ni Zamda A. John (Tanga), Christopher J. Emmanuel (Kigoma), Seperatus Lubinga (Iringa), Zuwena G. Abdala (Kusini Unguja) na Mgeni S. Mgeni (Kusini Pemba).
Mwenge wa Uhuru unatarajia kukamilisha mbio zake katika nchi nzima Octoba 14, 2013 mkoani Iringa utakapokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Ujembe wa Mbio za Mwenge mwaka huu 2013 unasema “Watanzania ni WamojaTusigawanywe kwa Misingi ya Tofauti Zetu za Dini, Itikadi na Rasilimali. Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni Ushindi wa Watanzania Wote. Mapambano Dhidi ya Rushwa, Ukimwi na Madawa ya Kulevya.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013
Next Post Previous Post
Bukobawadau