Bukobawadau

MKUU WA USALAMA CHAEDEMA WILFRED LWAKATARE SASA AHAMISHIWA MOI

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),amehamishiwa katika Kitengo cha Taasisi ya Mifupa(Moi) baada ya kutolewa katika wodi ya Sewahaji ambayo alilazwa awali kwa ajili ya uchunguzi.

Lwakatare ambaye anasumbuliwa na maumivu ya shingo yaliyosababishwa na kusagika kwa pingili mbili za shingo alifika hospitalini hapo Jumanne ya wiki hii, baada ya kuzidiwa na maumivu usiku wa kuamkia siku hiyo.

Akizungumza wodini hapo jana alisema alikuwa anasubiri ripoti ya madaktari ambao walikaa kikao cha kujadili tatizo lake na jinsi ya kulitatua hatua za awali zilizochukuliwa na kikao hicho ni kuhamishiwa kitengo cha mifupa Moi.

“Walivyokuja asubuhi(jana) baada ya kikao walinihamisha wamenileta huku na nimekabidhiwa daktari ambaye amepewa aniangalie na nimekabidhiwa namba yake hapa niwasiliane naye ndiyo nitajua nini kitaendelea huku,”alisema Lwakatare.

Alisema kwa sasa bado anasikia maumivu kwa mbali japokuwa amefungwa kifaa maalumu cha kuifanya shingo inyooke na kuzuia isichezecheze.

Katika uchunguzi uliofanywa juzi na madaktari ulionyesha kuwa hakuna njia zaidi yakuweza kumsaidia kupunguza maumivu hayo kama hatofanyiwa upasuaji wa kurekebisha pingili hizo.

“Hakuna kitu naogopa kama operesheni wakati ule ilikuwa pingili ya sita na ya saba ila sasa ni ya tatu na ya nne na nilishindwa kufanyiwa operesheni kipindi hicho kwa sababu niliona nikifanyiwa operesheni itanilaza na nitapoteza muda ila kwa sasa sina jinsi,”
Lwakatare sasa ahamishiwa Moi Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),amehamishiwa katika Kitengo cha Taasisi ya Mifupa(Moi) baada ya kutolewa katika wodi ya Sewahaji ambayo alilazwa awali kwa ajili ya uchunguzi. Lwakatare ambaye anasumbuliwa na maumivu ya shingo yaliyosababishwa na kusagika kwa pingili mbili za shingo alifika hospitalini hapo Jumanne ya wiki hii, baada ya kuzidiwa na maumivu usiku wa kuamkia siku hiyo. Akizungumza wodini hapo jana alisema alikuwa anasubiri ripoti ya madaktari ambao walikaa kikao cha kujadili tatizo lake na jinsi ya kulitatua hatua za awali zilizochukuliwa na kikao hicho ni kuhamishiwa kitengo cha mifupa Moi. “Walivyokuja asubuhi(jana) baada ya kikao walinihamisha wamenileta huku na nimekabidhiwa daktari ambaye amepewa aniangalie na nimekabidhiwa namba yake hapa niwasiliane naye ndiyo nitajua nini kitaendelea huku,”alisema Lwakatare. Alisema kwa sasa bado anasikia maumivu kwa mbali japokuwa amefungwa kifaa maalumu cha kuifanya shingo inyooke na kuzuia isichezecheze. Katika uchunguzi uliofanywa juzi na madaktari ulionyesha kuwa hakuna njia zaidi yakuweza kumsaidia kupunguza maumivu hayo kama hatofanyiwa upasuaji wa kurekebisha pingili hizo. “Hakuna kitu naogopa kama operesheni wakati ule ilikuwa pingili ya sita na ya saba ila sasa ni ya tatu na ya nne na nilishindwa kufanyiwa operesheni kipindi hicho kwa sababu niliona nikifanyiwa operesheni itanilaza na nitapoteza muda ila kwa sasa sina jinsi,”
Next Post Previous Post
Bukobawadau