Bukobawadau

PICHA ZETU ZA LEO #KIKWETU KWETU

Mdau msomaji unakumbuka nini na wapi kupitia picha hii
Taswira za makovu ya vita baada ya kuzuka vita Mwezi Oktoba 1978 ya Tanzania na nchi ya Uganda . Vita hii ilijulikana kwa jina maarufu la “vita ya Kagera” iliitwa jina hilo kutokana kwamba ilipiganiwa katika ardhi ya Tanzania mkoani Kagera. Vita hii ilisababishwa na kitendo cha Majeshi ya Uganda, chini ya Nduli Idd Amin Dada, kuvamia ardhi ya Tanzania katika eneo la Missenyi na kudai kuwa eneo lote lililo kaskazini mwa Mto Kagera ni ardhi ya nchi ya Uganda. Vita hivyo vilimalizika mwezi April, 1979 kwa Majeshi ya Tanzania kushinda vita na kumuondoa madarakani Nduli Idi Amini
Picha yetu ya leo #kikwetukwetu
Mdau akifanya yake, kama alivyokutwa na Camera yetu Kijijini Butembo-Muleba.
Next Post Previous Post
Bukobawadau