Bukobawadau

PROGRAMU YA KUKUZA AJIRA KWA VIJANA WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU.

PROGRAMU YA AJIRA Programu hii itatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu nchini,Taasisi za fedha na wabia wa maendeleo.Kwa kuanzia utekelezaji wake utaanza kwa kuendeleza programu ya mfano iliyoanzishwa na Idara ya kilimo, uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (DAEA-SUA) na hatimaye kuwafikia wahitimu wa vyuo vingine vya elimu ya juu katika kipindi husika. Kwa kuanzia serikali imekubaliana na Benki ya CRDB kuanza utoaji wa mikopo kwa vijana mara utekelezaji wa programu utakapoanza. Kwa kuwa kasi ya wanaojiunga elimu ya juu nchini imeongezeka wastani wa (48% kwa mwaka) na Wizara imeona vijana wanapomaliza elimu ya juu wanakuwa na elimu ya nadharia katika fani walizozisomea ,tumeona kuna umuhimu wa elimu ya ujasiriamli, mitaji na maeneo ya kufanyia uzalishaji na biashara ambavyo ni msingi wa programu hii. Programu hii ni bora kwa kuwa ina vigezo vya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji. MADHUMUNI YA PROGRAMU. Ni mojawapo ya hatua za utekelezaji wa sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 ya kuhamasisha uzalishaji wa kitaifa kufanikisha Ajira kamili yenye kipato na iliyochaguliwa kwa uhuru,kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira na ajira isiyokidhi viwango na kuongeza tija sehemu za kazi. LENGO: Lengo kuu la program ni kuongeza fursa za Ajira 30,000 za moja kwa moja kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na kuwawezesha vijana kujiajiri na hata kuajiri vijana wengine kutokana na miradi watakayoibuni wao wenyewe. Malengo mengine ni:- 1.Kuongeza idadi ya vijana wanaomiliki shughuli rasmi za kiuchumi na wamejiajiri na kuajiri wengine. 2. Kukuza utamaduni wa kijasiriamali pamoja na ubunifu. 3.Kuhamasisha matumizi bora ya nguvu kazi. PROGRAMU INALENGA. Programu hii inalenga vijana wa elimu ya juu ambao wapo tayari kuanzisha shughuli za kujiajiri katika sekta ya kilimo cha mazao, ufugaji, uvuvi, misitu na usindikaji. MIRADI. Miradi itakayoanzishwa itatoa ‘Mnyororo mzima wa thamani’ au INTERGRATED CROSS VALUE CHAIN (ICVC) Kwa mfano,mradi wa Alizeti na ukamuaji mafuta. 1st step- Uandaaji mashamba,ulimaji,upandaji,palizi na uvunaji 2nd step- Usafirishaji, uhifadhi, usindikaji 3rd step- Ukamuaji mafuta, ufungashaji na uuzaji mafuta. MAHITAJI YA RASILIMALI. Jumla ya shilingi bilioni 54.451 zitahitajika kwa kipindi cha miaka 3 ya utekelezaji wa programu ambapo shilingi Bilioni 50 zitawekwa dhamana na shilingi bilioni 4.451 zitatumika katika mafunzo na kuwaandaa vijana ili waweze kukopesheka MATOKEO YA PROGRAMU HII. I. Vijana watajengewa uwezo wa kujiajiri katika sekta zilizotajwa za kilimo,usindikaji,uvuvi na maeneo mengine kama vile viwanda vidogo na vya kati. II. Kuongezeka kwa fursa za Ajira nchini na kupungua kwa kiwango cha umaskini. III. Kupungua kwa matukio ya uhalifu na vitendo visivyokubalika katika jamii. IV. Kupungua kwa kasi ya vijana kuhamia mjini na kuimarika kwa uchumi wa nchi. MATOKEO TARAJIWA YA PROGRAMU. Programu hii ya wahitimu wa elimu ya juu itatoa fursa za Ajira kwa wahitimu 30,000 kutokana na miradi 1,000 kwa kipindi cha miaka 3. Uzoefu unaonesha kuwa mradi mmoja wa kilimo wenye thamani y ash. Million 50 una uwezo wa kutoa ajira kwa wahitimu 20 hadi 30. PROGRAMU ITATEKELEZA KATIKA AWAMU 3. (a) Awamu ya kwanza itahusisha vijana wahitimu 600 kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) kumiliki miradi 200 ya kujiajiri na kuajiri wahitimu wengine wasiopungua 5,400 kutoka maeneo mengine. (b) Awamu ya pili imelenga kuwawezesha vijana 900 wa elimu ya juu kutoka vyuo vingine ambao watakua tayari kuanzisha miradi ya kujiajiri na kuajiri wengine .Ambapo Miradi 300 itawezesha kuzalisha ajira za moja kwa moja kwa vijana wahitimu wasiopungua 8,100.Hapa miradi itahusisha sekta nyingine zitakazoonekana zina tija na kuongeza fursa za ajira. (c) Awamu ya tatu imelenga kuwawezesha vijana wahitimu 1,500 wa vyuo mbalimbali vya kati vikiwepo vya VETA. Jumla ya miradi 500 itawezeshwa na kuzalisha ajira kwa vijana 13,500. PROGRAMU ITAJUMUISHA YAFUATAYO. I. Utambuzi na uhamasishaji vijana—ambapowataandikishwa kupitia mikoa na Wilaya wanayoishi II. Kutoa mafunzo ya ujasiria mali na stadi zakazi-mafunzo yatatolewana SUA,baadae kwani kubuni na kuandaa andiko la Biashara (Business proposal) III. Kujenga uwezo wa vijana kulingana na miradi waliyoainisha –lengo ni kuwapatia ujuzi na uzoefuwa namna ya utekelezaji miradi. IV. Mafunzo na uzoefu kwa waendeshaji wa program-Wahusika watajengewa uwezo kujifunza kutokana na miradi ya ukuzaji ajira katika nchi nyingine.Taasisi husika Wizara ya Kazi na Ajira,Benki ya CRDB,SUA na SUGECO. V. Kutoa mafunzona huduma za kitaalamu na uratibu katika maeneo ya uzalishaji. UTARATIBU WA UKOPESHAJI. v Program hii ni ya miaka 3 na mikopo itakayotolewa ni ya miaka 3 na urejeshwaji wa mikopo ni kuanzia miaka3 hadi 5. v Muda wa mkopaji kurejesha mkopo ni kuanzia miezi 6 hadi mwaka 1 kutegemeana na aina ya mradi. v Utaratibu wa ukopeshaji ni wastani wa sh.Mil 50 hadi 300mil kulingana na mradi. Utaratibu wa utekelezaji na viwango vya riba utaainishwa katika mpango kazi wa utekelezaji
Next Post Previous Post
Bukobawadau