Bukobawadau

Awateka nyara maafisa wa Ujerumani

Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel amefuta mkutano wa kampeini yake uliopangwa kufanyika mji mmoja ulioko jimbo la Bavaria baada ya mwanamme aliyejihami kuwateka nyara watu watatu katika ukumbi wa baraza la mji.
Mashirika ya habari ya Ujerumani yanaripoti kwamba mwanamme huyo wa miaka 24 ana historia ya kuwafuata kisiri wafanyikazi wa baraza la mji.
Haijabainika masharti ambayo ametoa na polisi wamezingira eneo hilo. Miongoni mwa mateka ni pamoja na Naibu Meya.
Chancellor Merkel alitarajiwa kufanya mkutano wa hadhara nje ya medani kuu ya Bavaria katika misururu ya kampeini yake ya uchaguzi mkuu ujao
SOURCE: BBC
Next Post Previous Post
Bukobawadau