Bukobawadau

Habari kubwa kwa siku ya IDD Sheikh HUKO Kyela apigwa nondo akiswalisha..!!!


Kyela. Sikukuu ya Idd imeingia dosari wilayani hapa baada ya kuzuka vurugu iliyotokana na muumini wa dini hiyo kuinuka katikati ya ibada jana asubuhi kwenye msikiti mkuu wa wilaya mkoani Mbeya na kumpiga kwa nondo Sheikh wa msikiti wa wilaya, Nuhu Mwafilango.
Mbali na sheikh huyo kujeruhiwa mguuni na mkononi katika tukio hilo, watu wengine watatu wamejeruhiwa akiwamo Mweka Hazina wa Baraza la Waislamu (Bakwata) wa wilaya, Khamis Hussein aliyejeruhiwa kichwani na kwenye sikio.
Polisi mkoani humo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa watu sita wanashikiliwa na wanatarajiwa kufikishwa mahamani baada ya taratibu zote kukamilika.
Wakizugumzia tukio hilo baadhi ya waumini waliokuwapo kwenye ibada hiyo, walisema tukio hilo lilianza katikati ya ibada wakati waumini wote wakiwa wanaswali na ndipo ghafla waliposikia kelele za vurugu hizo.
“Tukiwa kwenye ibada na sheikh akiendelea kuongoza swala ndipo alipoinuka bwana mmoja akiwa ameshika kitu mfano wa nondo na kumpiga sheikh na vurugu zikaanza hapo na kusababisha watu wengine kujeruhiwa kwani yule mhalifu hakuwa peke yake, wengine waliibuka na kuanza kuwashambulia viongozi wetu wa msikiti,” alisema Idd Hussein.
Akizungumzia tukio hilo Katibu wa Bakwata Mkoa wa Mbeya, Juma Killah alisema vurugu hizo zimetokea baada ya baadhi ya Waislam kuhimiza mabadiliko katika mambo kadhaa huku Bakwata wakiyapinga.
“Hicho ni Kikundi cha Waislam ambao kimetoka Dar es Salaam na kuja huku Mbeya, kimeenea wilaya zote za Mbeya kwa lengo la kuleta machafuko na kutugombanisha na dini nyingine
Next Post Previous Post
Bukobawadau