Bukobawadau

NYOTA YA MAKAMBA KUNG'AA URAIS CCM - 2015

Na Aziz Msuya, Morogoro

VIONGOZI 105 kutoka vyuo vikuu 30 nchini, wamesema Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, ndiye mwenye sifa za kuwa rais kama atagombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wamesema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa kiongozi wa nchi ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani.

Matukio hayo ni pamoja na vurugu, watu wasio na hatia kutekwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.

Viongozi hao waliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wao ambao ulihusisha viongozi mbalimbali wa Serikali za wanafunzi katika vyuo vikuu.

Washiriki wa mkutano huo ambao haujaandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini (TAHLISO), ni Marais wa Vyuo Vikuu, Makamu wa Rais, Maspika, Mawaziri Wakuu na viongozi mbalimbali.

Katika mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro, viongozi hao walipendekeza jina la Bw. Makamba awe mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya CCM 2015.

Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya,

Bw. Theonest Theophil, alisema wajumbe walichagua majina matatu ya wagombea wa nafasi hiyo.

Majina hayo ni Bw. Makamba (CCM), Bw. Zitto Kamwe na Bw. John Mnyika wote kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

" M a j i n a h a y a n d i y o yaliyochomoza katika nafasi tatu za juu lakini jina la Bw. Makamba likapata kura 72, akifuatiwa na Bw. Kabwe aliyepata kura 20.

"Matokeo ya kura hizi, atapelekewa Bw. Makamba ambayekama akikubali kugombea, tutazunguka nchi nzima kumfanyia kampeni kwa sababu nchi hii kwa sasa inahitaji fikra mpya za kiongozi kijana...uchaguzi wetu haujaangalia itikadi za kisiasa wala dini," alisema Bw. Theophil.

Alizitaja sifa za kiongozi wanayemtaka kuwa kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.

Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu, asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viouvu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.

"Mkutano umeafiki kuwa, sifa zote Bw. Makamba anazo na ameonesha ujasiri katika nafasi za uongozi alizowahi kushika kwani ni mwadilifu, anakubalika na makundi yote ya vijana, wasomo na viongozi wenzake ndani, nje ya chama chake.

"Vijana sasa wameamka wanataka kiongozi kijana ambaye ataikomboa nchi yetu bila kujali itikadi yake kisiasa wala kidini," alisema Bw. William Kanyondo kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini, mkoani Arusha.

Bw. Theophil alisema kama Bw. Makamba atakubali kugombea kiti hicho na CCM ikakataa kumpitisha, watamshauri agombee kama mgombea binafsi.

Mkutano huo pia ulijadili masuala mengine ambayo ni tofauti ya kipato cha Watanzania na kudai hali hiyo ni ishara mbaya kwa amaninaum ojawaWatanzania.

Wal isem aukua ji w a uchumi bado haujaen da sambamba naahueniyamaishayaMtanzaniawa kawaid a, ubora w aelimu hasa vijijini na fursaz aaj ira.

Mkutan ohuoulian da liwanaTaasisi yaK upam bananaMaa dui watatuambaoni u jinga, m aradh i naumaski ni (FPI D)iliyopojijiniDar es Salaam

Next Post Previous Post
Bukobawadau