Bukobawadau

MDAU REGINA KAPINGA AKABIDHI MSAADA WA KOMPUTA NA VITABU SHULE YA MSINGI RUBAFU

 Taswira fukwe za bugabo  ziwa Victoria . Fukwe pekee ambayo bado haijatumiwa vya kutosha
Mdau mwenye upendo na mfano wa kuigwa Bi Regina Kapinga toka Bill and Melinda Gates Foundation Settle,uko USA akikabidhi msaada wa vitabu,computers na nguo kwa Watoto wa shule ya msingi Rubafu 'A' iliyopo kata ya Bugabo Wilaya ya Bukoba Vijijini ikiwa ni kumbukumbu ya shule aliyosomea ingawa kwa hivi sasa anaishi  nchini Marekani.
Jumla ya Vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Millioni 6 vimekabidhiwa.
Pia Bi Regnal ameweza kujitolea matengenezo ya  barabara yenye urefu wa km 3 ikiwa ni barabara ya kwanza katika eneo hilo tangu kuumbwa kwa sayari ya tatu ijulikanayo kama dunia.
Wanafunzi wa darasa la saba, shule ya msingi Rubafu wakipokea msaada wa vitabu na komputa.
Sehemu ya wadau wajumbe walio ungana na Bi Regnal Kapinga PHD watatu kushoto, pia anaonekana Mh Gidion diwani wa kata ya Rubafu wa pili kutoka kushoto.
 Mwanahabari Ndg Audax  Mtiganzi katika mahojiano  na Bi Regnal Kapinga.
Mdau mkubwa wa Utalii Bw William Oswald Rutta akiwa ameogozana na ujumbe kutoka Bill gate foundation akiwa maeneo ya Rubafu Bugabo akihojiwa na mwanahabari wa TBC Taifa kuhusu Mambo ya utalii.

Kiroyera Tours
www.kiroyeratours.com
www.kagera.org
www.budap.org
http://www.facebook.com/pages/Kiroyera-Tours-and-Consulting/171058592931255
http://www.twitter.com/kiroyeratours
http://www.youtube.com/user/kiroyeratours

Mandhali ya fukwe za bugabo
Hii inatufundisha wadau wa Bukoba tukumbuke hata shule za msigi tulizosomea,tuwawezeshe kwa kile kinachowezekana, sifa kubwa ya Buhaya ni Elimu sio Siasa! 
Next Post Previous Post
Bukobawadau