Bukobawadau

Msukosuko wa Sheikh ponda mpaka kupigwa Risasi kwa siku ya jana!

Shekh Ponda akisisistiza jambo mbele ya waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Kongamano , Augosti 10, mwaka huu mjini Morogoro 

Kutambulishwa jukwaani Shekh Ponda.
Askari wa FFU wakijisongeza kati kati ya uwanja mara baada ya muda wa kongamano kumalizika na huu ndio mwanzo wa patashika lililompata Sheikh Ponda
  Shekh Ponda akikaribishwa kwenye jukwaa kuu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege , mjini Morogoro
Shekh Ponda akisalimiana na Mhadhiri wa Mihadhara nchini, Ustaadhi Abubakari
Na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro. 
 KATIBU wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda, alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumizwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi kwenye bega lake la kulia wakati akiekelea katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya kumalizika kwa kongamano ya Dini ya Kiislamu.
Mkasa huyo ulitokea Jumamosi Augosti 10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la barabara ya Tumbaku karibu na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba , Manispaa ya Morogoro.
Shekhe  Ponda alishiriki katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani Morogoro na kufanyika siku ya Idd Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni ya siku hiyo. 
 Kongamano hilo lilipata baraka zote na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, ambalo lilitoa  masharti kadhaa ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni kutokashifu dini nyingine wala viongozi wa serikali. 
 Sakata la kutaka kutiwa mbaroni kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa kukiuka masharti ya Mahakama aliyopewa baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje wa  kutakiwa asitende kosa lolote la jinai anapotumikia adhabu hiyo. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai kuwa Shekhe Ponda baada ya kutoka ndani ya gari eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita chache katika barabara ya Tumbaku alitelemka na wakat akitaka kuingia garini ilifayuliwa risasi iliyompiga begani. 
 Ustaadh Msema alidai kuwa baada ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa wameambatana naye walimchukua na kumpakiza kwenye Piki Piki hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupoatiwa matibabu. 
 Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, baada ya kufika hospitali, waliona anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo walipoamua kumwondoa na kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda kuitaja. 
Akizungumzia kwa kina hali ya Shekhe Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu hai licha ya kuumia vibaya begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo jingine hususani Jijini Dar es Salaam kupata matibabu zaidi.
Alisema viongozi wa Umoja huo hauwezi kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa wakati huu ambapo kumekuwa na sinto fahamu.
Baadhi ya walinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe Ponda aliletwa hapo kwa usafiri wa Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya 50 na kuishia getini. 
 Walisema walimwingiza adi mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini waliamua kutoa taarifa Polisi kuwa wamevamiwa na watu ambapo muda si mrefu Polisi wa FFU waliwasili na gari lao Hospitalini hapo. 
 Hata hivyo walinzi hao walisema, baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe Ponda waliamua kumyanyua na kumbeba mabegani na kutoka naye mlango mwingine wakimlazimisha mlinzi kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa usafiri wa Pikipiki kusikojulikana. 
Kufikishwa kwa Sheshe Ponda katika Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na Mwenyekiti huyo ambaye alidai  kuwa waliamua kumwondoa baada ya kuchekewa  kupatiwa huduma. 
Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na Polisi na kufariki dunia. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilongine akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10, baada ya kutokea kwa tukio hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya kutokea kifo cha Shekhe Ponda. 
 “ Nimepingiwa simu zaidi ya 50 , zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia , ujumbe umesambazwa kwenye simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali hakuna kifo wala maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala hili” alisema Kamanda huyo. 
Juhudi za kufuatilia sakata la uvumi kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa kazi na Ripota a wetu huyu na usiku wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe Ponda yu hai isipokuwa ameumia vibaya sehemu ya bega . 
 “ Nipo katika eneo ambalo Shekhe Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo hatuwezi kupataja kiusalama , isipo kuwa ameumia vibaya kwenye bega lake. Lakini yu hai wala hajafa” alisema Msema. Polisi Mkoani hapa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo, nasi twaendelea kufuatulia kwa ukaribu.
 Umati wa waumini wa Kiislamu wakimsikiliza Shekh Ponda
 Waumini wa Dini ya Kiislamu wa mjini Morogoro wakimsikiliza Shekh Ponda
Waumini wa Kiislamu wakitawanyika uwanjani baada ya muda wa kongamano kufikia tamati,
Next Post Previous Post
Bukobawadau