Bukobawadau

RWAMISHENYE 2-1 KASHAI KWA MATOKEO HAYA RWAMISHENYE WATAKUTANA NA BILELE KATIKA FAINALI TAREHE 17 AUG SIKU YA JUMAMOSI ‪#‎KAGASHEKI‬ CUP 2013

 Uwanjani kaitaba   wanyaluganda wa kashai wakipiga jalamba

Ni wasaa wa timu zote mbili kuingia uwanjani

Timu zikiendelea kusalimiana

Wachezaji wakisalimiana muda mchache kabla ya mtanage kuanza

Utaratibu wa dua upande wa kashai
Hawa ni Rwamishenye wakifanya maombi pia.

Kikosi cha timu ya Rwamishenye kilichoanza



Timu ya Rwamishenye imeibuka shujaa na kufanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya KAGASHEKI CUP 2013 baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Kashai Fc katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Rwamishenye ndio walioanza kufunga bao kupitia mshambuliaji Khalid Seleman kipindi cha kwanza nao Kashai wakiongeza bidii na kuweza kusawazisha bao hilo kipindi hicho hicho cha kwanza kupitia mchezaji wao Paulo Manu.
 Mtanange ukiendelea hapa ...na hapa ni patashika kwenye goli la Rwamishenye..Timu ya Kashai ikisawazisha bao hapa kipindi cha kwanza..
Wachezaji wa Kashai wakishangilia baada ya kusawazisha bao na kufanya 1-1 dhidi ya Rwamishenye FC
Mashabiki wa Timu ya Kashai wakishangilia uwanjani Kaitaba 

Kipindi cha kwanza kikimalizika timu zote zikiwa nguvu sawa. Kipindi cha pili kilitawaliwa na timu ya Rwamishenye huku wachezaji wa timu ya Kashai Fc wakizembea kukaba wenzao na kuchoka ambapo  wachezaji wa Rwamishenye walitumia nafasi hiyo na kuweza kuwaongezea bao la pili kupitia mchezaji wao matata Hassan Hussein aliyeingia kipindi cha pili kwa mkwaju mkali uliompita mlinda mlango wa timu ya Kashai.

Askari walilazimika kusindikiza waamuzi wa mechi hiyo baada ya refa kumaliza mtanange huo uliochezwa dakika 90 tu na timu ya Rwamishenye ikiibuka kidedea kwa 2-1








Mashabiki wakiwa na mzuka mkubwa
hizi ni mbwembwe kabla ya mechi jamaa aamua kupiga lakaa zake mbili uwanjani akiwaombea kashai wapite  hatua ya nusu fainali, lakini mambo si mambo mpaka mwisho Kashai wametolewa kwa bao 2-1 dhidi ya Rwamishenye.
Ni full kalibatano!


Ushindi huu walioupata Rwamishenye unawawezesha kutinga hatua ya Fainali siku ya Jumamosi hii tarehe 17 Agosti kuwavaa washindi walioifunga timu ya Makhirikhiri (Kitendaguro Fc) jana ambao ni Bilele FC katika uwanja wa Kaitaba. 
 Mchezo huu pia umeweza kuingiliwa na sintofahamu baada ya mashabiki wa timu ya Kashai Fc kuanza kufanya vurugu na kurusha mawe dakika za mwishoni baada ya kuona timu yao imefungwa na jambo hilo limeweza kunyamazishwa na askari wa FFU waliokuwa uwanjani humo na kuweza kuwaokoa wachezaji na waamuzi wa mtanange huo wasidhurike.
Hapa ni furaha kwa timu ya Rwamishenye baada ya kupata bao la pili, anaonekana kiongozi wa timu hiyo ya Rwamishenye akicheza na mwendesha Baiskeli 
Mtangazaji Abdulrazak  Majid wa R Kasibante Fm Radio  88.5 akiwajibika.
Next Post Previous Post
Bukobawadau