Bukobawadau

BUKOBA:MSANII SHEMELA ASTAAFU MUSIC NA KUINGIA KATIKA SIASA!!!!

Pichani ni Mtangazaji wa Vision FM Radio Bukoba Bi Matrida katika interview ya tv show ya chanel 12 ya Wilayani Misenyi na msanii Shemela
 Msanii Shemela
Wakati baadhi ya wanasiasa wakiwa na mawazo ya kuachana na siasa baadhi yao wakidai inapoteza muda , hii imekuwa kinyume kwa msanii Shemela maarufu kama Shemela daima toka Kiziba Misenyi baada ya hivi punde kutangaza rasmi kuwa anaacha muziki na kuingia katika siasa.

Shemela anayetamba katika vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini na nyimbo mpya iitwayo malipo ni kesho,amesema ameamua kuingia katika siasa baada ya kuona baadhi ya wanasiasa wanaleta longo longo kibao hasa kijijini kwao Kiziba.
Pamoja na kuacha game la muziki Shemela anasema anajivunia mafanikio yake aliyopata mpaka sasa,ikiwa ni pamoja na heshima aliyonayo kwa jamii kutokana na kazi yake ya muziki,pia kupitia nyimbo yake ya kitambo kidogo iitwao Amenibamba amepata gari lake na sasa ana kiwanja ambapo ameanza kujenga nyumba yake.

Aidha shemela amewashauri wasanii wenzake kuwa, heshima na uvumilivu ni nguzo kuu katika mafanikio hivyo wasanii wakifuata hayo watafika mbali.

Shemela ni miongoni mwa wasanii waliopo ndani ya VISION MUSIC AMBASSADOR na Jumamosi hii Septemba 14,atafanya tamasha Bunazi Misenyi ikiwa ni show yake ya mwisho na atawaaga rasmi mashabiki wake wa Misenyi.

CREDIT:VISION MUSIC AMBASSADOR
Next Post Previous Post
Bukobawadau