Bukobawadau

GLOBAL PUBLISHERS YAKABIDHI MIL 15 MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA

Mkurugenzi wa Global Publishers, Masha Bukumbi akimkabidhi mfano wa hundi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Rosemary Lulabuka. Kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers Abdallah Mrisho, na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ukuzaji Rasilimali (TEA), Sylvia Gunze.
Masha Bukumbi akimkabidhi Rosemary hundi halisi.
Bukumbi akiwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha tamasha hilo na kueleza jinsi walivyotimiza ahadi ya kuisaidia elimu hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA akitoa shukrani baada ya kupokea hundi hiyo.

Na Richard Bukos
Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Championi, Risasi na Ijumaa Wikienda leo imeikabidhi Mamlaka la Elimu Tanzania (TEA) kiasi cha shilingi milioni 15, ambazo ni sehemu ya mapato yaliyopatikana kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7 mwaka huu.
Akipokea hundi ya fedha hizo kutoka kwa Mkurugenzi wa Global Publishers, Masha Bukumbi, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Rosemary Lulabuka aliishukuru kampuni hii kwa uchangiaji huo na kuziomba kampuni, taasisi, watu binafsi na wadau wengine kuiga mfano huo.
Rosemary amesema mpaka sasa mfuko wa mamlaka hiyo umekusanya jumla ya shilingi milioni mia tano na kuwashukuru wadau wote waliochangia ambapo kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni kwa kujenga mabweni 30, ya Shule ya Sekondari ya Kibaigwa ambayo yatatumika na wanafunzi wapatao 1504.
Mkurugenzi huyo ameiomba Kampuni ya Global Publishers kuliendeleza tamasha hilo kila mwaka na kuwaomba wadau watakaoshirikishwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwani lengo lake kuu ni kukuza elimu hapa nchini jambo ambalo ni ukumbozi wa taifa letu.

(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

Next Post Previous Post
Bukobawadau