Bukobawadau

LIVE:MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA KARUME ENGLISH MEDIUM BUKOBA SEPTEMBA 14,2013

Pichani anaonekana Mgeni Rasmi Mr Katemana (katikati)akiingia eneo la tukio , kulia ni Mkurugenzi wa shule ya Karume Day&Boarding Mr Self Mkude.
Shule ya Karume English  Medium hivi sasa inaaminika na imejizolea umaarufu toka mwaka jana ilipo ongoza Mkoani kwa matokeo mazuri ya darasa la saba na uwenda historia ikajirudia
Mama Mkude pichani kushoto akiongea na mmoja wa wazazi  aliyehudhulia mahafali haya leo tarehe 14 sep.2013 sambamba na kumtolea maelezo kadha wa kadha
Kwa Mwaka  jana 2012,Mkoani Kagera shule ilioongoza ni KARUME DAY&BOARDING,Shule hii ilikuwa ya kwanza kiwilaya na ya kwanza kimkoa kati ya shule 984.
Kitaifa ikawa ya 6 kati ya shule 15,051.Shule ya Karume inaongozwa na Mkurugenzi Mr Mkude na kwa sasa inakaribisha wanafunzi wapya kwa mwaka 2012 kuanzia darasa la awali mpaka darasa la sita.

Fomu zinapatikana Karume Day&Boarding iliopo maeneo ya Nshambya au kituo cha shule kilichopo Kashai Matopeni.
Kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga simu
+255 754 658055
+255 754 608324
+255 719 614155
Email;karumecenter@yahoo.co.uk

Utapata fomu kwa haraka sana

Heka heka za hapa na pale zikiendelea mapema hii shuleni hapa.
Maandalizi ya msosi ndiyo kwanza yanaanza.
 Wazazi na baadhi ya wanafunzi na wanafunzi  wakiwa katika hali ya utulivu
 Bukobawadau tupo eneo la tukio, hivyo endelea kuwa nasi kwa picha na maelezo zaidi ya kile kinachojili.
 Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Karume English Medium
 Kutoka eneo la Kyabitembe  kwa mbali ni muonekano wa  maeneo ya Kabale, kitwe , kiziru na Kibeta.
Muonekano wa viwanja vya shule ya Karume English Medium
Mdau Sadi Idd akiwa na mwanae pichani anayehitimu hii leo
Waalikwa wakiendelea kuingia eneo la tukio
Katikati ni Bi Shamila Ismail wa Kamachumu , mmoja wa wazazi waliohudhulia mahafali haya.


Muonekano nadhifu wa mwanafunzi
 Kaka Mkuu ni mmoja wa  wageni waalikwa akisaini kitabu cha wageni
Sehemu ya meza kuu.


 Muda wa msosi
Uongozi wa Karume Day&Boarding unawakaribisha sana.

 Bukobawadau Blogspot tunawapongeza wanafunzi wote walio hitimu shuleni hapo na tunampongeza Mdau wetu Ndg Self Mkude.
INAENDELEA

Next Post Previous Post
Bukobawadau