Bukobawadau

Chuo Kikuu Dodoma sasa kutoa stashahada


Dodoma. Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimeanza kukabiliana tatizo la kushuka kwa idadi ya  wanafunzi wanaodahiliwa mwaka hadi mwaka kwa kuanzisha kozi cheti (certificate) na stashahada (diploma).
Hayo yalisemwa mkoani hapa na Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo hicho ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Baraza jipya.
Profesa Kikula alisema kwa kunzisha programu hizo kutasaidia kukabiliana changamoto hiyo kwa kupata idadi ya wanafunzi wanaotosheleza miundombinu iliyopo.
“Ni dhamira yetu kuwa programu hizi zitasaidia kuongeza wigo wa udahili wa wanafunzi na pia kuongeza kipato cha hapa chuoni,” alisema Kikula.
Pia alilitaka baraza hilo kushauri menejimenti ya chuo njia mbadala za kutatua changamoto zilizopo. Alisema kwa kufanya hivyo kutawawezesha wanafunzi kupata sifa za kujiunga na chuo kikuu hicho.
Jumla ya wanafunzi 494 wamedahiliwa katika programu hizo zilizoanza mwaka huu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi alilitaka baraza hilo kushughulikia ipasavyo kero za madai mbalimbali ya wafanyakazi.
“Pia baraza la wafanyakazi linatakiwa kuhakikisha linafanya vikao vyake inavyotakiwa kisheria ili kuepuka migogoro isiyo na lazima."
Next Post Previous Post
Bukobawadau