Bukobawadau

Gaidi aliyelipua TANZANIA na KENYA 1998 akamatwa

(Abu al Liby ©FBI/Reuters)
Mtuhumiwa wa ugaidi aliyehusika na shambulizi la kulipua balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998, Abu Anas al Liby ameripotiwa kukamatwa nchini Libya, ikiwa ni siku chache tokea shambulizi la ugaidi nchini Kenya kwenye maduka ya Westgate.

al Liby anmbaye anatajwa kuhusika moja kwa moja kwenye shambulizi la mwaka 1998 ambalo liliua zaidi ya watu 220, amekamatwa na oparesheni ya ghafla na vikosi vya hali ya juu vya jeshi la Marekani, Navy Seal, CNN imeripoti.
Kwa mujibu wa Reuters, oparesheni mbili za namna hii zimefanyika siku ya jana nchini Libya pamoja na Somalia, ambapo hii ya Libya imeleta mafanikio, huku ya nchini Somalia ikiwa haijazaa matunda kutokana na kutompata waliyekuwa wanamtafuta (ambaye hata hivyo hawajataka kumtaja jina).


(Mmojawapo wa komandoo wa jeshi la Mareakani akilinda eneo baada ya mlipuko kwenye ubalozi wa Marekani jijini Nairobi mwaka 1998. Mshukiwa wa tukio hilo, Abu Anas al Liby, amekamatwa nchini Libya Jumamosi tar 5 Oktoba.)

Kwa hivi sasa Abu al Liby ameshikiliwa na kupelekwa nje ya Libya, ambapo msemaji wa makao makuu ya idara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, George Little amesema kuwa, yuko salama, ila wasingependa kutaja ni wapi kutokana na sababu za kiusalama.
Kukamatwa kwa al Liby ni hatua kubwa kwenye vita dhidi ya ugaidi duniani, ambapo kwa muda mrefu Marekani ilikuwa ikimtafuta, na kuahidi kitita cha dola milioni tano kwa mtu yeyote atakayefanikisha

Source : Reuters
Next Post Previous Post
Bukobawadau