Bukobawadau

Hatma ya Barasa kwenda ICC kujulikana leo Kenya

Fatou Bensouda,mwendesha mashtaka mkuu wa ICC huko The Haque
Mahakama moja nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi  Ijumaa  juu ya ombi la mahakama ya kimataifa ya uhalifu- ICC kutaka kukabidhiwa kwa mwanaharakati Walter Barasa. Mahakama hiyo yenye makao makuu yake The Haque inamshutumu mtu huyo kwa kuingilia mashahidi.
 
Barasa anakanusha shutuma hizi kuwa hazina msingi. “Sina wasi wasi  kwa sababu ninakanusha shutuma zilizoelezewa dhidi yangu, na zaidi ya hayo wakili  wangu ana maelezo na ataelezea hilo wakati ukifika, alisema Barasa”.

ICC ilitoa kibali cha kukamatwa dhidi ya Barasa  lakini  aliwasilisha changamoto dhidi ya amri ya  kukamatwa katika mahakama ya Kenya. Wakili wa upande  wa utetezi wa Barasa, Kibe Mungai aliishutumu ICC kwa kudharau katiba ya Kenya. Anasema kwa mfano kesi yake inatakiwa kusikilizwa katika mahakama za Kenya, na pia kwamba hatua ya ICC inakiuka haki yake ya katiba ya kuona ushahidi dhidi yake.

Walter Barasa

“Bwana Barasa anataka mahakama itangaze  kwamba serikali ya Kenya haiwezi kutekeleza ombi la ICC”,  alisema Mungai. “Kama akifanikiwa  huo ndio mwisho wa habari. Kama pia anafanikiwa  kwa upande mwingine kwamba kesi ifanyike nchini  Kenya, basi  suala la hati ya  kukamatwa linafikia tamati. Kama hatoshinda basi huwenda akajisalimisha kwa ICC”.
 
Mungai anasema kama mahakama inafuata katiba ya Kenya mteja wake hastahili kukabidhiwa kwa ICC. Alisema wote ICC na Kenya walikosea walipotoa hati ya  kukamatwa kwa Barasa.“Tuna nafasi nzuri”, alisema Mungai. “ICC imekuwa ikishughulikia suala hili kinyume cha sheria na  Kenya kama taifa  imeitafsiri vibaya  sheria katika kutoa ombi la kutaka ajisalimishe”.
 
ICC ilimshutumu Barasa kwa kuwahonga mashahidi katika kesi ya Naibu Rais wa Kenya, William Ruto. Mahakama inamshutumu bwana Ruto na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kuwa wahusika  wakuu katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya wa mwaka 2007-2008 ambazo zilisababisha kiasi cha watu 1,300 kufariki na maelfu kukoseshwa makazi ndani ya nchi. Barasa anakanusha mashtaka ya ICC.

Wakili  wa upande wa  utetezi, bwana Mungai anasema hati ya  kukamatwa iliyotolewa na ICC dhidi ya Barasa inakiuka katiba ya Kenya

VOA
Next Post Previous Post
Bukobawadau