Bukobawadau

IRON LADY LOVENESS MAMUYA AZIDI KUIPEPERUSHA BENDERA YA CCM MAENDELEO NA UZALENDO ZAIDI

Na Alex Kassuwi wa Swahili TV/Radio
Hakuna siyetambua mchango wa Mwanamke Jasiri na Shujaa Iron Lady Loves Mamuya kwa mchango wake katika chama tawala CCM. Itakumbukwa kwamba Loveness Mamuya ndiye alihamisha Ufunguzi wa matawi ya CCM hapa Marekani.

Baada ya pendekezo la ufunguzi wa matawi ya nje hapa Marekani lililowasilishwa na Mheshimiwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Siasa, Ndugu, Nape Moses Mnawiye.November, 11, 2011 Loveness hakusita alienda mbele na mara moja kufungua
Tawi la Washington DC, Maryland na Virginia tarehe August 25, 2012 na Mheshimiwa Abrahamani Kinana ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa alikuwa mgeni rasmi.

Iron lady aliweza kuliongoza Tawi hili kwa mafanikio makubwa kwa muda wa mwaka mmoja, na hatimaye kuzaa mashina ya Hystiville one, Lanham one. Loveness hakuishia hapo aliendelea kufanya kazi usiku na mchana kwa kushirikiana na wana CCM wenzake na kufanikiwa kuitanua CCM katika majimbo ya Marekani, Ambapo Mhe. Mwigulu Nchemba  Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Taifa alikuja na kuwa mgeni rasmi na kufungua pamoja na kuyabariki matawi hayo, ambayo ni California, DMV, Ohio, Texas, Chicago na North Carolina.

Swahili Radio na TV iliweza kuongea na Iron Lady Loveness Mamuya na alikuwa na haya ya kusema;

" Vijana tujitokeze tusikae nyuma, umoja ni ushindi, tujiunge na chama tukose pale palipokosewa tujenge na kuitangaa nchi yetu" Iron Lady ameongeza pia
"Kama kijana leta mchango wako tusikae nyuma tusonge mbele na tuwe mabalozi wazuri nyumbani na ughaibuni"
Kwa kumalizia Iron Lady ametoa wito kwa vijana kwamba vijana tutumie ujana wetu vizuri tusipoangalia  tutaiharibu nchi yetu wenyewe kwa ushabiki usio na maana na tutapogundua tuliharibu  hatutakuwa vijana tena.
Next Post Previous Post
Bukobawadau