Jaji Warioba afafanua kauli ya Bulembo
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa ufafanuzi kuhusu kauli mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi wa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya iliyomalizika hivi karibuni. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Oktoba 3, 2013), Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba amesema siku zote Tume yake imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwataka wanasiasa hao kujadili rasimu iliyotolewa badala ya Tume au Wajumbe wake.