Bukobawadau

KITUO CHA RUSUMO MKOANI KAGERA 'CHAFUMULIWA'

Katapila liking'oa miti iliyokuwa karibu na ofisi za uhamiaji mpakani Rusumo tayari kabisa kuanza kwa ujenzi wa kituo kipya kitaalamu kinajulikana kama OSBP.
Kituo cha Uhamiaji Rusumo mara baada ya kusambaratishwa kupisha ujenzi wa OSBP
Ofisi ya Uhamiaji Rusumo ikiwa imesambaratishwa
Ofisi za muda za TRA mpakani Rusumo
Ofisi ya muda inayotumiwa na Uhamiaji, TRA na idara nyingine za serikali katika mpaka wa Rusumo
Ujenzi wa barabara ukiendelea
Kituo cha Uhamiaji na Idara nyingine za serikali katika mpaka wa Rusumo zimebomolewa na kuhamishiwa sehemu nyingine kupisha ujenzi wa kituo kipya cha Kisasa cha kutoa huduma mpakani maarufu kwa OSBP (One Stop Border Post).

Ujenzi huo unaosimamiwa na kampuni moja ya Kijapani umeanza rasmi wiki hii baada ya kumaliza kuhamisha vifaa na mitambo mbalimbali ya ofisi hizo.

Akiongea na Blogger wetu aliyekuwepo mpakani Rusumo, Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji Mrakibu wa Uhamiaji Ndugu Mahirane alisema ‘’Tulikuwa tunasubiria wataalamu wetu wa IT kutoka Makao Makuu ambao wamefika leo hii na tayari wameshahamisha mitambo yetu ya Kompyuta, na kama unavyoona wajapani walipoona tumemaliza kutoa vifaa wakaanza na ubomoaji wa majengo ya zamani. Nadhani kama kweli watakuwa na spidi waliyonayo sasa hivi basi baada ya mwaka tutakuwa na jengo jipya hapa mpakani’’.

Nao maofisa wa idara nyingine walionesha kufurahishwa na hatua hiyo ya kujengwa kwa kituo kipya cha huduma za mpakani kitakachokusanya idara zote.
Next Post Previous Post
Bukobawadau