Bukobawadau

MZEE PIUS NGEZE ATIMIZA MIAKA 70 YA KUZALIWA KWAKE *MISA TAKATIFU YA KUMSHUKURU MUNGU YAONGOZWA NA BABA ASKOFU KILAINI NDANI YA KANISA KUU BUKOBA CATHEDRAL*

 Pichani anaonekana Mzee Pius Ngeze na Mke wake Bi Rechol Ngeze katika ibada ya  misa takatifu ya kumshukru Mungu,ambapo leo tarehe 19. Octoba. 2013 Mzee Ngeze  ametimiza umri wa miaka 70 ya kuzaliwa kwake.


Ndugu wadau pichani ni tukio kamili lililofanyika leo  tarehe 19.10.2013, Mzee Pius Ngeze wa Mjini Bukoba, ameandaa  ibada ya kutimiza miaka 70 ya kuzaliwa kwake vivyo hivyo kesho  tarehe 18.10.2013 atazindua azindua kitabu cha maisha yake, kitabu hicho kimeandikwa na Padre Privatus Karugendo mbaye ni rafiki mkubwa wa familia ya Mzee Ngeze.
Mzee Pius Ngeze pamoja na kulitumia taifa na chama chake cha CCM kwa uaminifu mkubwa, ni mtu anaheshimika sana kwenye jamii inayomzunguka na Tanzania nzima. Huyu ni miongoni mwa wazendo wa nchii hii! Lakini pia huyu ni msomi anayeshirikisha elimu yake kwa watanzania wote. Hadi sasa hivi ameandika vitabu zaidi ya 66, vya kilimo na ushirika. Pia ni mchapishaji wa vitabu ambaye anachapisha vitabu vya elimu na kuwahamisisha wazee wa mkoa wa Kagera, kuandika historia ya maisha yao.




Ibada takatifu ikiendelea.
Mhashamu Methodius Kilaini,  Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba akiongoza ibada ndani ya Kanisa Kuu Jimbo katoliki la Bukoba


Mzee Pius Ngeze katika picha ya pamoja na familia yake.
Mzee Ngeze katika picha ya pamoja na rafiki wake wa karibu Padre Privatus Karugendo.


Kwa wadau waliopo mjini BukobaWatakao mnaombwa kufuatilia fuatilia kwa ukaribu tukio hili la  kihistoria. 
 Mzee Pius Ngeze katika picha ya pamoja na Askofu Kilaini.
 Baba Askofu Kilaini katika picha ya pamoja na Mr & Mrs Ngeze.



Timu nzima ya Bukobawadau Blog tunaomba wadau nyote tushirikiane kumpongeza Mzee wetu Mwana wa Tanzania na Afrika, kwa kufikisha miaka 70 ya kuzaliwa na Mwenyezi Mungu amwongezee miaka mingine ya kuishi!!!

Next Post Previous Post
Bukobawadau