Bukobawadau

PRESS RELEASE

Profesa Mohammed Y. Janabi (pichani) , Daktari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanikiwa kuingia katika kundi dogo la madaktari wa Afrika waliothibitisha kuwa na ujuzi na utaalam wa kuwapima na kutoa liseni za vipimo vya afya kwa watumishi wa anga wakiwamo marubani.

Katika barua ambayo aliipokea Dkt. Janabi wakati anaandamana na Rais Kikwete katika ziara ya kikazi ya Marekani na Canada iliyomalizika leo, Jumamosi, Septemba 28, 2013, Wizara ya Usafirishaji ya Marekani kupitia Utawala wa Shughuli za Anga wa Marekani (FAA) imesema kuwa imemteua Profesa na Dkt. Janabi kuwa Daktari wa Shughuli za Anga (AME) kuanzia Agosti 14, mwaka huu, 2013.

“Uamuzi huu una maana kuwa sasa unaweza kuwapima na kuendesha shughuli za kitibabu na kutoa ama kukataa kutoa liseni ya kuthibtisha afya za watumishi wa sekta ya anga wakiwemo marubani wa ndege za usafirishaji, wa ndege za biashara za abiria, marubani wa ndege binafsi na marubani wanafunzi.

Profesa Janabi anakuwa daktari wa 31 katika Afrika na wa tatu katika Afrika Mashariki kupatiwa hadhi hiyo ambayo inapatikana baada ya kazi ngumu ambayo ni pamoja na kufanya mtihani maalum.

Nchi pekee katika Afrika Mashariki iliyokuwa na madaktari wa kiwango hicho kabla ya Dkt. Janabi kuingia katika kundi hilo ni Kenya yenye madaktari wawili. Tanzania sasa inakuwa nchi ya pili katika Afrika Mashariki kuwa na hadhi hiyo.

Kwa upande wa Afrika, Profesa Janabi anaungana na madaktari kutoka Burkina Faso (1), Cameroun (2), Misri (6) ambayo ndiyo madaktari wengi zaidi katika kundi hili, Ghana (1), Libya (1), Morocco (1), Nigeria (5), Ethiopia (4), Kenya (2), Afrika Kusini (5) kukubaliwa kuifanya kazi hii ya kimataifa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
 29 Septemba, 2013
Next Post Previous Post
Bukobawadau