Bukobawadau

WAZIRI KAGASHEKI ALIFUNGUKIA JESHI LA POLISI

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki amesema vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watumishi wa jeshi la polisi bado ni kikwazo kwenye mapambano dhidi ya ujangili.
Amesema licha ya watuhumiwa kukamatwa na vithibitisho lakini bado wengi hususani raia wa kigeni wamekuwa wakiachiwa na hivyo kuhamasisha vitendo hivyo kuzidi kushamiri.
Licha ya kuanzisha operesheni maalumu ya kamata majangili yenye lengo la kudhibiti mauaji ya tembo lakini baadhi ya watumishi wa jeshi la polisi wameendelea kuwa kikwazo katika mapambano hayo.
Waziri Kagasheki anasema operesheni hiyo yenye baraka zote za Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Rais Jakaya Kikwete itaendelea licha ya wahujumu hao kuingilia juhudi hizo, huku akiahidi kuwachukulia hatua za kisheria watakapobainika.
Aidha katika oparesheni hiyo ya kamata majangili baadhi ya watumishi wa wizara hiyo wamebainika kuwa washirika wa biashara hiyo haramu.

JIUNGE NA UKURASA WETU MPYA WA FACEBOOK KUPITA LINK HII  KWA HABARI ZA PAPO KWA PAPO GONGA: https://www.facebook.com/Bukobawadau
Next Post Previous Post
Bukobawadau