Bukobawadau

CHUKUA MUDA WAKO KUSOMA MKASA HUU ULIOMKUTA DADA HUYU MREMBO WA NGUVU KUTOKA ARUSHA ALIYETENDWA NA MDOGO WAKE...!

MIMI ni mwanamke mwenye umri wa miaka 24 nna umbo zuri watu wananisifia kila napopita, kuhusu elimu nimehitimu chuo mwaka juzi.. Mimi kwakweli mpaka sasa naumia nafsi kila nikikumbuka alichonitendea mdogo wangu.

Kwani ni mdogo wangu wa damu kabisa na nilimuamini kwa kila kitu yani sikuwahi kufikiri kwamba siku moja atanitenda, Jina langu naitwa Nancy nimezaliwa katika familia ya

watoto sita wakiume wanne wakike tupo wawili Nyumbani ni arusha kabila ni mmeru.

Nimeamuwa kumsimulia mwandishi wa tovuti hii yamasainyotambofu.com na hii jamani ni Stori ya kweli naombeni ushauri kwa yeyote atakaeguswa na mkasa huu, Katika pitapita za kimapenzi nilifanikiwa kukutana na mvulana Fundi Computer mitaa ya posta jijini dar wakati nikiwa masomoni IFM, Bwana huyo alifahamika kwa jina la 'Deju', Deju alikuwa mwanaume mtiifu na mwenye kunijali nitake nini asininunulie?.. Kila nilichotaka alininunulia labda vilivyo nje ya uwezo wake tu ndio alishindwa kuninunulia.

Nilimtambulisha kwa marafiki zangu wote na ndugu wote maana mara nyingi wakati wa likizo tulifunga safari kuelekea nyumbani kwetu Arusha kuwasalimia ndugu zangu, Dar Es Salaam nilikua naishi kigamboni kwa mamkubwa na baada ya hapo niliamua kupanga chumba ambacho nilisaidiwa kulipa kodi na mpenzi wangu ili tuwe huru katika mapezi yetu, Ila cha ajabu yeye hakuwahi kunipeleka kwao wala kunitambulisha kwa mmoja kati ya nduguze...!


 Aliishia kuniambia tu kwamba kwao ni dodoma mpwapwa, Sikujuwa kwamba Deju atakuja kugeuka nyoka mwenye sumu kali ya kuniathiri maishani mwangu..! Mwanaume huyu nimedumu nae kwa muda wa takribani miaka mitatu ikafikia kipindi namuacha na mdogo wangu wanatoka nae mimi napumzika wnaenda waendako wanakula bata mpaka basi, wakati huo mdogo wangu alikuwa akiishi gongo la mboto kwa Rafiki yangu wa kike ambye ni mwanamitindo. Kwahiyo kila wikiend alikuwa akija kunitembelea nyumbani kwangu ndipo Deju alipopatia fursa.

Wakati mwingine tunaweza tukatoka wote lakini akawa benet na mdogo wangu kuliko mimi..! Mpaka watu wasio tujua wanahisi wao ndio wapenzi mimi ni msindikizaji, Lakini mimi sikuweza kuhisi kitu maana mimi namdogo wangu tunaheshimiana na yule mwanaume hakuwahi kunionyeshea uhuni wowote zaidi ya siku moja iliingia messege ya namba iliyoseviwa Kibaka mzoefu alafu messege imeandikwa JUZI
ULINIKOLEZA MPENZI.. NIMEMIC MAHABA YAKO. Nilipomuuliza akanijibu kwamba huwenda kuna rafiki yake aliitumia simu yake huwenda alisahau akasevu namba na mwanamke wake,

Basi nikamuamini, Kumbe ananivutia pumzi, Sasa siku niliyosulubiwa mambo yalikuwa hivi.

Mdogo wangu aliniaga kwamba anaenda Arusha kusalimia alafu atarejea baada ya siku tatu Nikamkubalia, kesho yake alfajiri nataka kumsindikiza akaniambia dada we pumzika huu ni muda wako wa kumpetipeti mumeo. Nikamwambia haya wasalimie.

Akaianza safari kama kawaida kumbe safari yake inaishia Sinza katika hoteli moja ambayo sio vizuri kuitaja kwani hata nikiitaja bado sio Dawa, Basi kwakuwa mwanaume wangu wakati mwingine alikuwa akilala nyumbani kwake ilala sikuweza kushtuka kwamba kuna kamchezo, Kumbe Alishampa hela ya kulipa chumba cha hoteli siku tatu ili wakajichane,..! Tulivyoamka nikamuandalia maji ya kuoga babyboy wangu kama kawaida tukanywa chai, baada ya hapo akaelekea kazini kwake kama kawaida.

Ilivyofika saa kumi na moja alasiri mwanaume akanipigia simu na kuambia kwamba amepata dharura ya kikazi kuelekea morogoro atanijuza siku inayofuata kwamba atarudi lini, mimi nikakubali nikamtakia safari njema na busu kwenye simu juu mmmwaaaaaa... kumbe anaelekea Sinza mdogo wangu na babyboy wangu walinifanyia ndivyosivyo..

Namshukuru sana rafiki yangu kipenzi Patrisha kwa kunitonya kamchozo nilikochezewa na mdogo wangu na mwanaume wangu mpaka sasa japo mapenzi yangu mimi na Deju yamekwisha lakini nipo huru.

 Nilishangaa napigiwa simu na patrisha nikaenda eneo la tukio na kuwakuta wakilishana Ndizi rost..! Nilipoteza fahamu na kujikuta nimezingirwa na watu huku nimeloa maji. Nipeni ushauri niwe na mpenzi mwingine kwa sasa au nitulie kwanza?

Nancy
Next Post Previous Post
Bukobawadau