Bukobawadau

MKOANI KAGERA HUYU NDIYE BIBI MWENYE UMRI MKUBWA NI BI STERIA NYANGOMA ALIFREDI IKWATAKI



Pichani ni Bibi Steria Nyangoma Alifred Ikwataki anayesadikika kuwa na umri mkubwa kwani inasadikika ana umri wa miaka 117, kimaisha anaishi Wilayani Karagwe  ndani ya kata ya Ihembe, kijiji cha Ihembe II  ndani ya familia ya Mzee Ikwatika maarufu kama 'Ta Ikwatika'.
Bukobawadau Blog tupo katika jitihada za kuitembelea familia hiyo ili tuweze kupata maelezo yanayojitosheleza.
 Muonekano wa nyimba anayoishi Bibi Steria
Pichani ni Mtoto wa 2 wa kuzaliwa kwa Bibi Steria ajulikanaye kama Mzee Christian Binemungu Ikwataki, mwenye umri wa miaka 78 mpaka hivi leo ,kikubwa kwake ni kwamba anao wanawake wanne|(4) na jumla ya watoto 36 wa kuwazaa.
Pichani kutoka kushoto ni Mjukuu wa Bibi huyo Mdau Audax Mganyizi Ikwataki, katikati ni Bi Marry arkipo ikwataki ambaye mke wa Mtoto wa nne kuzaliwa na Bibi Steria naye ni Mzee Arkipo Ikwataki pichani kulia mwenye umri wa miaka 71 ya kuzaliwa .
Next Post Previous Post
Bukobawadau