Bukobawadau

MSHAMBULIAJI KAGERA SUGAR AWAPIGIA SALUTI WAKALI WA KUFUMANIA NYAVU LIGI KUU BARA!!

MSHAMBULIAJI hatari wa Kagera Sugar, Themi Felix mwenye magoli 7 kwa sasa amewakubali washambuliaji wenzake wa ligi hiyo kuwa wako vizuri sana na wanastahili pongezi kwa uwezo wao mkubwa..

Akizungumza na mtandao wa FULLSHANGWE, Felix ambaye alikuwa anawania tuzo ya mwanaspoti bora wa mwaka inayoandaliwa na gazeti la michezo la Mwanaspoti amekiri kuwa waliomtangulia katika mabao wanaiweza kazi na yeye anapata changamoto kubwa zaidi.

“Kuna washambuliaji kama Amisi Tambwe wa Simba, Khamis Kiiza wa Yanga, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar, hakika wanaweza kazi na wanaonesha uwezo wa hali ya juu kufumania nyavu, lakini na mimi najipanga vizuri zaidi ili kuendelea kupambana nao”. Alisema Felix.

Ferlix aliongeza kuwa ligi ya mwaka huu imekuwa ngumu sana na ukizingatia imekuwa na vijana wengi wenye uchu wa kupata mafanikio.

Pia alisema kuwa timu ndogo kama Mbeya City zimebadili sura na mtazamo wa ligi yetu, ingawa wasiwasi wake ni kuwa mzunguko wa pili hana uhakika kama watahimili mikikimikiki ya vigogo Simba na Yanga.

“Kwa ligi yetu na utamaduni wa timu zetu, sina imani kama Mbeya City wataendelea kuwepo kule juu, lakini nisiseme sana kwani unaweza kusema hawatakuwepo kumbe wakawepo, tusubiri kuona itakuwaje”. Alisema Felix.

Felix alisema kwa sasa wamevunja kambi, lakini yeye akiwa mchezaji anaendelea na mazoezi ya kujiweka sawa kwani akikaa tu atajikuta anaanza upya.
Next Post Previous Post
Bukobawadau