Bukobawadau

CHECK CAMERA YETU IKIANGAZA KIJIJINI BUGANGUZI MULEBA DECEMBER 2013

Kijiji cha Bushemba Kata ya Buganguzi Wilaya ya Muleba,Camera yetu inakutana na mdau pichani,mfanyabiashara ya ndizi akiwa katika ukusanyaji wake kabla ya kuzipeleka Sokoni.
 Maeneo ya kijiji hiki cha Bushemba Buganguzi , hii ni  mojawapo ya eneo linalochangamka sana,Center maarufu kwa jina la 'AKAUMULA'
 Akaumula Center.
 Mvua zikinyesha hali ya barabara kijijini ni shida!!
 Camera yetu uso kwa uso na mjengo huu, ukiwa umeota vyema katikati ya migomba
 Camera yetu ikiangaza huku na kule.
 Mwanalibeneke najisogeza nyumba ya jirani ili kutaka kujua ni nani mdau anaye endeleza ujenzi wa nyumba inayo onekana hapo juu!!
 Naambiwa hizi ni jitihada za Mdau Thobard Theonest.
 Muonekano wa nyuma wa Nyumba hii hakika Ndg Thobard anastahili pongezi.
 Home sweet Home.
Ndg Theobard Theonest ni mzaliwa wa kijiji hiki cha Buganguzi ila kwa sasa makazi yake yapo Jijini Dar es Salaam, Bukobawadau Blog tumefurahishwa na jitihada zako mzee.
 Hali halisi ya maisha ya Kijijini.
 Mdau msomaji popote ulipo tuanze sasa safari yetu ya pamoja kutafakari hali na mustakabali wa maisha ya kijijini  kwetu na kwenu.
 Tukikuangazia mtaa kwa mtaa ndani ya Kijiji cha buganguzi
Masikani kwa Mdau Majid (baba wawili)
Kusimama barabarani ni matokeo ya maisha ya mwananchi wa Kijijini, pamoja na changamoto kubwa za ukosefu wa huduma muhimu
Kupitia Bukobawadau Blog unapata taswira ya maisha yetu ya zamani kijijini.
Hapa na pale na Camera yetu ndani ya kijiji cha buganguzi
 Buganguzi Center maarufu kwa jina la 'Buganguzi akona'

Leo tena inatulazimu kutembelea  Nyumba hii yenye kila sifa ikiwa na ziada ya uwanja wa basketball
 Miaka miwili iliyopita, Camera yetu ilifika hapaNyumbani kwa Mdau Alex Mtiganzi,Kijijini  Kabulala-Buhanga  Buganguzi umbali wa km 2 kutoka Buganguzi  Center.
Bustani safi yenyekupendeza hakika bukobawadau Blog tutaendelea kumpongeza Mdau Alex Mtiganzi kwa kupenda nyumbani  kwa vitendo.

Nyumba imezungushiwa uzio mkubwa
Mwonekano wa kanisa la Kilutheri lililopo kijiji cha Buganguzi.

Next Post Previous Post
Bukobawadau