Bukobawadau

NUKUU YETU LEO DEC 17,2013

 Wakati mke wa rais Obama akiwa chuo, kulikuwa na wanawake wachache sana wa kiafrika katika chuo hicho..
Hivyo akapewa mwanachumba mwenzake ambaye ni mzungu, na mama wa yule binti wa kizungu alijisikia vibaya baada ya mtoto wake kumwambia anashea chumba na binti wa kiafrika aitwaye Michelle. 

Mama yule kwa hasira kali akauendea uongozi wa shule na hatimaye Michelle akahamishwa na kutoka katika chumba kile.
Lakini leo, yule binti ambaye hakuwa na hatia yoyote amekuwa THE FIRST LADY wa USA (mke wa rais wa Marekani). 

Katika kitabu ambacho kimechapishwa hivi karibuni kuhusu maisha ya Michelle, yule mama wa kizungu aliyekataa mtoto wake asikae chumba kimoja na Michelle, alihojiwa na akakubaliana kuwa alifanya hivyo na sasa anaumizwa kwa kitendo kile na kukijutia
NUKUU YETU NI KWAMBA mtu au watu wanaokukataa leo na kukuponda, kesho watasherehekea mafanikio yako kwa njia moja ama nyingine
Next Post Previous Post
Bukobawadau