TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
BUKOBAWADAU
5 Dec, 2013
TAARIFA YA AJALI YA MOTO KATIKA OFISI ZA CHADEMA
NDUGU WANAHABARI, MNAMO TAREHE 03/12/2013 MUDA WA SAA 5:00 ASUBUHI,
POLISI MKOANI HAPA TULIPOKEA TAARIFA JUU YA KUCHOMWA MOTO KWA JENGO
AMBALO LINA OFISI ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
ZILIZOPO MTAA WA NGARENARO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA.
MARA
BAADA YA TAARIFA HIYO ASKARI WALIKWENDA KATIKA ENEO LA TUKIO NA KUKUTA
MOTO UMEZIMIKA. JENGO HILO AMBALO LINA UZIO MREFU WA MATOFALI NA GETI
MOJA LA MBELE LINA OFISI TATU ZA CHAMA HICHO AMBAZO NI OFISI ZA WILAYA,
MKOA NA KANDA YA KASKAZINI AMBAZO ZINATUMIA BAFU NA CHOO KIMOJA.
AIDHA UCHUNGUZI ULIOFANYWA NA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA ZIMAMOTO IMEGUNDUA MAMBO YAFUATAYO:-
KWANZA, OFISI HIZO ZINALINDWA NA WALINZI WA CHAMA HICHO “RED BRIGADES”
NA SIKU YA TUKIO MLINZI ALIYEKUWA ZAMU ALIKUWA KITUMBWIZI S/O BAHATI
(42) MKAZI WA OLASITI AMBAYE ALIINGIA KAZINI TAREHE 02/12/2013 MUDA WA
SAA 12:00 JIONI NA KUTOKA TAREHE 03/12/2013 MUDA WA SAA 12:00 ASUBUHI.
AIDHA OFISI HIZO ZINA KATIBU MUHTASI MMOJA AITWAYE JENIFER D/O MWASHA
(25) MKAZI WA SOMBETINI AMBAYE UWA ANAINGIA KAZINI SAA 1:30 ASUBUHI KILA
SIKU LAKINI SIKU YA TUKIO ALIINGIA SAA 4:00 ASUBUHI.
PILI,
UCHUNGUZI UMEENDELEA KUBAINI KUWA, HAKUNA MAHALI PALIPOVUNJWA KUTOKA
KWENYE UZIO WA OFISI HIZO KURUHUSU MTU/WATU KUINGIA NDANI.
TATU, MLANGO WA NYUMA WA OFISI HIZO KATIKA VERANDA KULIGUNDULIKA TUNDU
KATIKA DARI KUELEKEA BAFUNI TUNDU LENYE UPANA WA FUTI MOJA NA NUSU KWA
NUSU (11/2X1/2) AMBALO NI DOGO KIASI CHA KUTOWEZESHA MTU KUPENYA KUINGIA
NDANI YA OFISI HIZO.
NNE, NDANI YA BAFU KULIPATIKANA MAJIVU NA KWENYE SAKAFU NA JUU YA SINKI YAKIWA MAKAVU BILA MAJI MAJI YOYOTE.
TANO, KUTA ZOTE ZA BAFU NA CHOO HAZIKUWA ZIMEUNGUA.
SITA, ENEO LILILOUNGUA KWENYE DARI NI 3/4 (ROBO TATU MITA) LENYE UPANA WA MITA 1 KWA UREFU WA MITA 3.
SABA, ENEO AMBALO MOTO ULIONEKANA UMEWAKA, MBAO KATIKA DARI ZILIONEKANA
KUUNGUA UPANDE WA CHINI NA UPANDE WA JUU WA MBAO NA CEILING BOARD
HAZIJAUNGUA KUOMYESHA MOTO ULIANZIA CHINI.
NANE, KUMEPATIKANA
KIPANDE CHA CHUMA KILICHOKUWA NA KARATASI ZILIZOUNGUA PAMOJA NA TOCHI
NDANI YA DARI ENEO AMBALO MOTO ULIKUWA UKIWAKA LAKINI VITU HIVYO
HAVIKUONYESHA DALILI ZA KUUNGUA AU KUSHIKA MOTO, NA INAONYESHA VIMEWEKWA
BAADA YA MOTO KUZIMWA.
TISA, KUNA UWEZEKANO MKUBWA MOTO HUO ULIZIMWA KWA KUTUMIA HEWA CHAFU/CO2.
KUFUATIA TUKIO HILO JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA KUWAHOJI MLINZI WA
OFISI HIZO KITUMBWIZI S/O BAHATI PAMOJA NA KATIBU MUHTASI JENIFER D/O
MWASHA, HUKU UPELELEZI ZAIDI JUU YA TUKIO HILO UKIENDELEA. ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) JAPHET LUSINGU
TAREHE 04/12/2013.
BUKOBAWADAU
Bukoba Wadau ni mtandao unao toa habari na matukio yanayo tokea katika mji wa bukoba pamoja na mkoa wa kagera kwa ujumla.
Email:bukobawadau@gmail.com | Phone :Mc baraka:0784 505045, 0754 505043
Instagram @bukobawadau | Facebook @bukobawadau