Bukobawadau

TASWIRA MAPOKEZI /MAZISHI YA MAREHEMU HATIFU GALIATANO YALIYOFANYIKA LEO 6 DEC,2013 KIJIJINI BUGANGUZI MULEBA.

Ni Majira ya saa saba mchana wa Dec 5,2013 ndege ya shirika la Precission Air ikiwasili uwanja wa ndege Mjini Bukoba.
Ndege hiyo ikiwa na abiria mbalimbali pamoja na dada ndugu wa marehemu Hatifu Galiatano,wakiwa wamefika kushiriki katika msiba huu na ndugu zao wengine wengi waliojikita kimaisha mjini hapa,Pichani katikati ni anaonekana Dr . Hanath ambaye ni dada mkubwa wa marehemu.
Dr. Anath akiwa ameongozana na dada yake mkubwa Bi Hausa Ismail pichani kushoto wanapokewa na wana ndugu wengine akiwepo Mh. Mwajabu na Haji Sadick.
 Msiba umefanyikia Rajab House, masikini kwa mzee Galiatano
 Mzee Selemani wa Kishanda alifika kumfariji Mzee Galiatano
 Ndugu wa familia wakiteta jambo.

Nyumbani kwa Mzee Haji Abbakari Rajabu Galiatano,katikati ya mji wa Bukoba,barabara ya tupendane ndipo ulipokua msiba huu, ambapo wanandugu wote waliweza kuomboleza na kufarijiwa na marafiki  wa familia jamaa na viongozi wengineo wa chama/vyama na serikali.
 Bi Jeanifer Murungi Kichwabuta akisalimiana na mzee
 Sadick,Nurag na Khalid wakisikilizana
 Mc Baraka, Jeanifer na Dr Hanath.
Baada ya hapo familia nzima ya wafiwa ikaelekea kijijini Buganguzi kwa ajili ya mapokezi ya mwili wa Marehemu na mazishi.
Vilio vikitawala mala baada ya kuwasili mwili wa Marehemu Nyumbani Buganguzi,kama anavyo onekana Mzee wetu Haji Abbakari Galiatano akiwa kwenye simanzi na huzini mkubwa!!wadau niwaombe tuendele kumfariji mzee huyu katika kipindi hiki cha majonzi!!
Mjane wa Marehemu Hatifu uso kwa uso na wanae, ni vilio kwa kiasi kiasi kikubwa.
 Mwili wa marehemu Hatifu Galiatano ukipokelewa nyumbani kwao kijijini Buganguzi.
 Waombolezaji wakiuingiza mwili wa marehemu ndani.
Vilio na huzuni kwa kila mtu.
 Huzuni mkubwa umetanda.
Sehemu ya waombolezaji , katikati ni Ndg Razack Issack.
 Mzee Balyagati akitoa salaam za rambirambi kutoka CCM Wilaya Missenyi.
 Ndugu Sadru Hassani akitowa wasifu wa marehemu Hatifu Galiatano.
Salaam za rambirambi kutoka Jijini Dar es Salaam zikitolewa na Ndg Ismail.
 Haji Abuba Sued akitoa salaam za rambirambi kutoka jumuhiya ya wazee wa Mkoa Kagera
 Shughuli hii iliwezwa kuratibiwa na kusimamiwa vyema na Sheikh Idrisa, na hapa akiwaomba watu kusimama kama ishara ya heshima kufuatia kufika kwa Sheikh Mustapha.
 Hivi ndivyo anavyo ingia Sheikh Mustapha.
 Haji Hashim Mgunda akimlaki Sheikh.
Kwa mahaba makubwa ile wahaya wanasema 'Obujune no Obuchulezi'sheikh anahanguka kifuani kwa shwahiba wake Mzee Galiatano!


 Sheikh Haruna kichwabuta akitoa nasaha zake zilizoweza kushika, kugusa na kubaki hakilini mwa mamia ya wadau walioweza kushiriki shughuli hii ya mazishi.
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Sheikh kwa umakini mkubwa, yupo mzee Pius Ngeze, Mzee Balyagati, Mzee Kanatti pia mzee Yasini anaonekana pichani kulia kabisa.
Macho na masikio yote kwa Sheikh Haruna Kichwabuta wakati akiendelea kutoa nasaha zake.

Viongezi wadini wakimsikilia Sheikh Haruna.
Hawa ni wadau Wenyeji wa kijiji hiki cha Buganguzi.
Taswira mbalimbali katika shughuli ya mazishi ya Marehemu Hatifu Galiatano iliyofanyika jioni ya leo 6 Dec.2013 nyumbani kwao kijijini Buganguzi
Wadau wakimsikilisha Sheikh Haruna Kichwabuta.
Mzee Galiatano, Mzee Abduziad Kashinde na Mzee Abuba Sued Kagasheki.
Mzee Kakobe wa Nshamba Muleba pichani kulia.
 Mama Rugusha akisikilizana na Mama Hachi Mnyonge.
 Mama Chaltina Angelo Mshana na Mama Merry Rwabizi.
Marehemu Hatifu amemwacha mjane pichana na watito wawili hawapo katika picha hii.
 Kulia ni Shangazi wa Marehemu, Mama Zuliath Rajabu Galiatano.
Sehemu ya wanamama waliofika kuwafariji wafiwa.


 Ndg Salum Galiatano pichani
 Swala ya kuswalia Maiti ikiongozwa na Sheikh Mstapha.
Katika hali ya upweka Maiti ikiswaliwa nje ya nyumba  na huo ndio mwanzo wa safari ya kuelekea makaburini kwa maziko.
 Maiti ikiingizwa kaburini.
 Sheikh Mustapha akisogezewa udongo,
 Sheikh Mustapha akiweka udongo kaburini
 Shughuli ya mazishi ikiendelea
Mzee Tibaigana akishiriki kuweka udongo.
 Waombolezaji wakishiriki shughuli nzima ya mazishi.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya mji wa Bukoba Ndg Anathory Amani akishiriki katika mazishi haya.
Shughuli ya mazishi ikiendelea.
 Mdau Yusuph Songoro.
Sheikh Zakhria, Sheikh wa wilaya ya Muleba akiweka udongo kaburini
Shughuli ikiwa inaendelea....
Hivi ndivyo ilivyokua safari ya mwisho kwa ndugu yetu  Marehemu Hatifu Galiatano mwenyezi mungu ailaze roho yake mahala pema
Mdau Mzee Tibaigana akiteta jambo na Dada Merry.

Wanafamilia wakibadilishana mawazo baada ya shughuli ya mazishi.
Wakati hili likiendelea na kuna mengine uendelea...!
Ndugu Nuru Galiatano pichani kushoto akiongea na Mkodomi wake.
 Ndg Frank pichani kushoto akitolea jambo ufafanuzi.
Katika hili na hili 
Mdau Khalid na Dr. Hanath hwa ni ndg wa marehemu,wakiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa watoto wa Marehemu Hatifu.
 Shukrani kwako Ndg Malick Tibabimale kuendeleza mshikamano na familia hii.
Ndugu na jamaa wa familia ya Haji Galiatano.

 Mdau Badlu,Hanifa, Rausa na Dada Najiath.
Mdau Mama Farida
Hamidu, Badlu, Mzee Tiba na Haji Nurag.
Kamanda Ghaspa akifanya yake.
Mdau Hamis , Deo, Bashiru Badae na Ndg Yakubu.
Tupo bega kwa bega na Mdau Jamal Karumuna.
Mh. Anathory Amani pembeni ni Ndg Hamza Itembwe.
Mdau Eunice Luangisa
 Dada Passy akitoa mkono wa pole kwa mzee Galiatano.
Uncle Issack akisalimiana na Mzee Galiatano.
Mzee Pius Ngeze akipata huduma ya chakula.
Fursa ya msosi
Upande wa jikon mambo yalikuwa kama hivi.
Bi Jeanifer Murungi Kichwabuta, Bro Majid na Mzee Nurag wakiwajibika.
Sehemu ya Maegesho.
 Sehemu ya wadau wakisikilizia kwa mbali.

BUKOBAWADAU BLOG TUNASEMA MSIBA  HUU NI WETU SOTE NA TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA.

 ... Allah atatupa mioyo ya subra sote twatakiwa tuseme Inna Lilah wa Inna Illah raj unn!!!

Next Post Previous Post
Bukobawadau