Bukobawadau

FURAHIA BUKOBA YETU LEO JAN 28,2014

Muonekano wa Mji wa Bukoba kwa Juu, maeneo ya Uswahilini Bilele,na mitaa ya Hindu.
 Sehemu ya Mji wa Bukoba unavyoonekana kutokea juu
 Maeneo ya stand kuu mjini hapa.
 Nyumba makazi ya mdau.
 Uwanja wa ndege Mjini bukobaBukoba ambao umepanuliwa pamoja na kuwekewa lami.
Usawa wa mwisho wa uwanja wa ndege mjini Bukoba
Muonekano usawa wa mwanzo wa Uwanja wetu wa Ndege.
 Ujenzi wa Jengo jipya la abiria bado unaendelea.
 Zifuatazo ni picha mbalimbali za mandhari ya Mji wetu,furahia Bukoba kupitia Bukobawadau Blog.
 Ofisi ya Mhola Bukoba,
 Camera yetu uso kwa uso na Mdau Bob Anderson mitaa ya kati mjini hapa.
Ni kweli bila ya shaka, BUKOBA ni mji mzuri.
Kupitia BUKOBAWADAU BLOG unaweza kujionea mpangilio mzuri wa mji huu ambao umejengwa kwa kuzungukwa na milima yenye rangi ya kijani kibichi.
 Mandhari safi na mpangilio safi wa mji huku upande mmoja ukiwa umeachwa wazi bila mlima

 Kwa uumbaji huu Wadau tuendelee kumtukuza Mwenyezi Mungu muumba wetu kwa fursa anayotupa ya uhai na kushuhudia uumbaji wake.
 Kivutio kingine ni jengo hili la Halmashauri ya Bukoba Vijijini,Halmashauri yenye historia kabla ya Uhuru wa Nchi yetu.
Team Bukobawadau tunasema  Asante Mungu wetu!!!


Next Post Previous Post
Bukobawadau