Bukobawadau

CHECK MWISHO WA SALAAM ZA HERI YA MWAKA MPYA '2014' KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI JAN 16,2014

Hi Wadau, ninawatakia baraka za mwaka mpya ili mipango yenu iweze kufanikiwa. Ukiwa na shughuli ya kiburudani usikose kuwasiliana na KAKAU Band Bukoba, KAPOTIVE Star Singers-Bukoba. Andrew Kagya.
 Elice Msamila:mm namshukuru mungu sana kwa kunifikisha mwaka huu 2014 salama na familia yangu,nawapenda wote wanaonipenda na wasio nipenda.ila namuomba mungu sana mwaka huu atubadilishe mioyo yetu tuweze kumtumikia vema.kifupi naitaji AMANI sana ktk maisha yangu ukiwa na Amani kila kitu utapata kupitia Amani!
Ashraf Lugusha; Inakuadje fanz wangu wa nguvu...ebana nafurah sana na nnashkuru kwa support ambayo nimekuwa nikiipata kutoka team nzima ya BUKOBA WADAU BLOG, najpanga vzr so soon mambo mapya na makali zaid yanakuja stay tuned mashabiq wang & HAPPY NEW YEAR!!!!
 I thank you for creating ths amazing blog that brings light in and out our town and to my life in general. Keep up with the good work that make change in our daily basis..Happy# 2014 kwa wadau wote. Mungu ibariki Bukoba wadau kwa ushirikiano mzuri. Naitwa Salmin Saleh kyaishozi.
 Innocent Deus;Hakika Mungu ni mwema,Nashukuru  kwa kunipa afya njema kuweza kufika mwaka mpya 2014 nikiwa katika hatua nyingine na mpya  katika maisha yangu.
Naitwa Godfrey Rugalabamu ila najulikana zaid kama McGaraB. The Best Mc in Different Occasions &Events..2013 imekua,ya Baraka sana kwa upande wangu namshukuru Mungu sana kwa hilo kwa mengi mazuri alionitendea .Nikitarajia makubwa zaidi kwa mwaka huu 2014!Nikiamini katika kile nnacho kifanya.Massage yenu kwenu wadau wa Bukobawadau Blog inasema hivi. Do not give up om ur Dream ,work on it na hakika utafanikiwa tena kwa mwaka huuhuu 2014 ukiamua sasa.. Sema 20-4-teen is 20-4-Me!Over Ukiitaji huduma zangu call.0714/0767 637457 Email. godfrey@mcgarab.com Web. www.mcgarab.com Asanteni sana.
Happy Amos.Ujumbe nawatakia watanzania Wenzangu  heri ya Mwaka  wa mafanikio
Mimi kama Dada Kabendera mtangazaji wa kituo cha RBA....Rwanda Broadcasting Agenc....Radio and TV...nawatakia Wa Tz wote hasa wadau wa Bukoba kheri ya mwaka mpya na mafanikio mema... tufanye kazi kwa bidii ili kujikuza kimaendeleo kwani majungu hayajengi yanabomoa...
Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika mwaka 2014 Nawatakia mema wadau wote ktk mwaka huu.Letty
 Omutwale Innocent Mushaijaki kutoka Ishozi Rutala lakini kwa sasa naishi jijini Dar es salaam na kufanya kazi katika kampuni ya SCANAD kama media monitoring meneger,nawatakia heri na fanaka katika mwaka huu mpya wa 2014 na pia nasema kwamba TWETOHYE TULEKELE OLWANGO , OKUTENDELANA N'ENOBI.
 2014 is a brand new year. Forget about the past, Live your Brand New Life,Take chances,Be crazy sometimes and work very hard.Dont waste ur time to please people,thats old shit.Do what is right for u,No body walks in your shoes "The only person that can save u is u" Happy New Year.Shamila Ismail.
Mdau Buberwa Robert,Nawatakia heri ya mwaka mpya 2014 watu wote duniani. Ujumbe wangu tuweke amani mbele. Watanzania tuwe wabunifu na si walalamishi
Regica Rwamulege na mumewe G.Rwamugira. Ujumbe: Tunawapenda wote hatubagui rangi wala Kabila. Tunaipenda Tanzania zaidi ya yote, tunawamiss Wadau wa Bukoba
Mdau Mwesiga Johnstone;New Years marks a new beginning. New people to meet, new adventures to enjoy and new memories to create. Here's wishing you the Happiest New Year ever!
Levis Lupondije a.k.a DUBE Nawatakia heri ya mwaka  mpya 2014A, Maisha ni kupambana tu, tukaze buti hakuna kulala, haijalishi uko wapi na unafanya nini kwa wakati  upi.'HAPPY NEW YEAR 2014
Sarah Katarama,May you all be blessed with joy and happiness all the year round....Happy new year 2014.
 Rita Laurent na Goreth Laurent tunatoa salaam za heeri ya mwaka mpya kwa Ndugu Jamaa Na Marafiki, tuna shukuru Sana Mc Baraka kwa kutuweka karibu na Nyumbani Bukoba tunapata Habari nzuri kutoka bukoba na picha zenye kuvutia , tumefurahi sana kwa moyo huo na wale wanao sadia kufanikisha hii blog kuendelea vizuri mpaka sasa.Tunashuru sana
Naitwa Julius Lubega;Mwaka huu hatuhitaji kumtafta mchawi, Nawatakieni 2014 wa tukijua kudharau ni chanzo cha umasikini. Peace to you bukobawadau blogsport God bless. 

Ndugu Murshid Hassan Byeyombo
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Maruk Vanilla Farming and Processing Ltd

Ndugu Wadau,

Kwa niaba ya Wakurugenzi wa Maruk Vanilla Farming and Processing (MVFP) Ltd nawatakia mwaka mpya wenye heri na mafanikio katika mipango yenu. Sisi kama MVFP Ltd tunawaahidi kuendeleza gurudumu la ukombozi wa Mkulima wa Vanilla na mazao mengine ya Biashara hasa viungo (spices).

Mwishoni mwa mwaka jana tulianzisha mpango maalumu wa kuongeza uzalishaji wa zao la vanilla kwa kugawa marando (vines) mapya. Pia tuliweza kuanza ushamirishaji wa mazao mbadala ya Biashara mkoani mwetu. Tumeweza kugawa zaidi ya miche 7500 ya vanilla na miche 800 ya pilipilimanga (black pepper) yote kwa wakulima wapya. Mpango huu umeonyesha kuitikiwa vema na wakulima hivyo mwaka 2014 tutazidisha jitihada.

Mwaka huu tayari tumezindua huduma ya MALIPO YA AWALI KWA WAKULIMA WENYE DHARURA. Huduma hii ni maalumu kuwakwamua wakulima wa vanilla kifedha wakati wakisubiri mavuno na mauzo ya mazao yao. Dharura zitakazo hudumiwa ni zile zinazohusiana na Elimu na Afya kwa wanafamilia wa mkulima wa vanilla. Tunatarajia kupanua mkondo mmoja wa huduma hii kufikia kuwa huduma kamili ya Bima ya Afya kwa Wakulima.

Kama ilivyo ada, msimu wa mwaka huu 2014 MVFP Ltd itaendeleza sera yake ya manunuzi ya vanilla kwa mkulima ambayo wakulima hulipwa papo kwa papo pesa taslimu mara tu wanapofikisha mazao yao kwenye kituo cha manunuzi. Tunaheshimu utaratibu huu kwani tunatambua kuwa mkulima anauza mazao yake ili kujikomboa na kukidhi mahitaji mbalimbali. Kwa kuwa mahitaji na shida zake hazisubiri baadae, hivyo malipo kufanyika muda kitambo baada ya mauzo ni kumfanya mkulima ashindwe kutimiza haja zake. Na hatma yake wakulima huacha kuhudumia mashamba, hung’oa miche na kulichukia zao. 

Kuna kila dalili kwamba bei ya mapodo itapanda na hivyo kumfanya mkulima apate malipo mazuri. MVFP Ltd tunazidi kuwasisitiza wakulima kuongeza uzalishaji na kujali miche yao. Pia tunaishauri serikali na wadau wa maendeleo kumulika zao hili la vanilla. Tuna imani kwamba vanilla ina uwezo mkubwa wa kubadili maisha ya wakulima iwapo itapata msukumo stahili kutoka kwa wafanya maamuzi na watendaji wa vyombo vya umma.
 Mwisho tunapenda kuwashukuru na kuwapongeza wamiliki na waendeshaji wa http://bukobawadau.blogspot.com/ kwa kazi nzuri wanayoifanya kuuhabarisha umma juu ya nini kinaendelea nyumbani na duniani. Blog hii imetusaidia kwa njia ya “trickle-down effect” ambapo wale walioko mbali na nyumbani, baada ya kusoma habari zetu hapa, huamasisha walioko nyumbani kujiunga na kilimo cha vanilla. Tunaomba wadau muendelee na moyo huu kwa maendeleo ya watu wetu na Kagera yetu.

 
Obyjr Obyemarila Byeyombo:Heri na fanaka ya mwaka mpya 2014 na uwe mwaka mzuri kwetu sote wa mafanikio, upendo, amani na mshikamano kwa sote ameen. Ujumbe: Vyema kukusanyika kwa mwoyo wa dhati na kushirikiana katika kuonyeshana njia za kuboresha maisha, kuliko kukusanyika kwa unafki na kunywa kula huku tukivimbiashana vifua kuonyeshana nani mwenye pesa kuliko mwenzie. Mabadiliko ya kweli yanatakiwa kwa WAHAYA wote hayo magari mnayokodisha na kuazima ama hata kununua ila kwa lengo la kwenda Bukoba town katika season kujionyeshea ni bora mjenge nyumba za mama zenu na baba zenu huko vijijini au mziwekeze apo town hayo ndio maendeleo ya kweli, kiroho safi tubadilikeni
 Each new day is a blank page in the diary of your life. The secret of success is in turning that  diary into the best story you possibly can. I wish you Happy New Year and diary full of best stories ever written in your life. SUKA LYRICS 2014.
 Salaam Za Heri na Fanaka ya Krismasi na Mwaka Mpya 2014 kutoka Kwa Deo Mugoa,Toronto Canada
 Belinda Rugarabamu A.k.a mwanaharakati..Nawatakia Heri ya mwaka mpya 2014 familia yangu na watu wote wapenda maendeleo. Ujumbe-Tuache majungu makazini,tupige kazi kwa bidii maana majungu c mtaji!
 Hodi hodi, naitwa Lilian napenda kuwatakia wana bukoba wote pamoja na ndugu jamaa na marafiki heri ya mwaka mpya, Mungu awajalie baraka tele. May we experience lot of it in this 2014 also i thank bukobawadau blog for your effort, guys hav done a good thing kufungua hii blog kweli tunaona mambo mengi yanayoendelea bukoba hadi raha. shukrani sana and all the best in 2014.. God bless
Salma Komba (mama frank) Nawatakia heri ya mwaka mpya wa Tanzania wote popote walipo ujumbe tudumishe amani tulionayo.
 Siraji Majura kutoka Kemondo;Ujumbe Maisha yakikupiga chenga Ruksa kucheza Rafu!
Finally 2013 Came To An End. Happy New Year For All Of U.As the Year Goes on, You are also get old Before leaving let me Wish you All for You Good Future and full of success as the last year was very challenging but still we belive we can still make it with our life goals as i belive where theirs a will theirs a way,so just axcept the challanges and make sure your playing a right game to achive the success.And also thanks alot mc for updating us withl all the news around the world ,bukoba we are one.Rehena Gulam.
Naitwa Alpha Rwirangira mshindi wa Tusker Project Fame S 3....mwaka 2009....na Tusker All Stars 2011...kwa sasa nipo marekani kimasomo,kupitia Bukobawadau Blog nawatakieni Heri ya Mwaka Mpya 2014
Annah Kyungay; “Anyone who has never made a mistake has never tried anything new” 2014 Jipange.
Ninapenda kutuma salam za heri ya ya Mwaka mpya kutoka London England kwa familia ya baba yangu Mdogo Mr Emanuel Kagya (BKB club) na familia yake. From Denis L Mugizi.
  On behalf of my family....I wish you all the best on the occasion of the New Year’s Day,. Hope this 2014 brings new inspiration to mind and bring lots of happiness in ur life. Best of luck to all my friends, relatives and all found in Bukoba especially my mom, young sister Penina and my best friend Maja although i'm not there but our soul and heart are still together.Justine Cyprian, Dar
 Naitwa Vann Vanessa,Napenda kuwatakia  wadau nyote heri ya mwaka mpya 2014.
 Kokubelwa Kamaleki kutoka  Karagwe nawatakia ndg ,jamaa na wadau wote heri ya mwaka mpya.
 Oscar;Ninawatakia kheri ya mwaka mpya 2014, uwe mwaka wa mafanikio kwa watanzania wote, aman na upendo iwe slaa yetu..... mungu ibariki BUKOBA, MUNGU ibarikiTANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA NA ULIMWENGU KWA UJUMLA....


NOTE;KUPATA MATUKIO YA JANA AU YA MUDA MCHACHE ULIOPITA TUNAKUKUMBUSHA KUPITIA 'OLDER POST'KILA MWISHO WA UKURASA WETU, KUPATA UPDATE KUPITIA EMAIL YAKO JIUNGE NASI KWA KUWA FELLOW/MEMBER KWA KUJOIN NASI  PEMBENI KULIA MWA BLOG YETU.


Next Post Previous Post
Bukobawadau