HUKO BUNDO BABA WA MIAKA 54 AOA MTOTO WA MIAKA MINANE
Bunda. Polisi Wilaya ya Bunda, wanamshikilia baba mwenye umri wa miaka 54 kwa tuhuma kuoa mwanafunzi wa kike wa umri wa miaka minane.
Msimamizi wa Dawati la Jinsia katika Kituo Kikuu
cha Polisi Bunda, Rita Charles alisema baba huyo mkazi wa Kijiji cha
Nyaburundu wilayani Bunda alikamatwa jana akiwa anaishi na binti huyo
(jina limehifadhiwa) kama mke wa nyumbani baada ya kutoa kishika uchumba
kiasi cha Sh55,000 kwa wazazi wake.
Ilielezwa kuwa mwanaume huyo kabla ya kumwoa mtoto
huyo aliyekuwa anasoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi
Nyaburundu, alimchumbia kwa wazazi wake na kutakiwa atoe ng’ombe watano
za mahari ndipo akatoa kishika uchumba hicho na mtoto huyo kuondolewa
shule. “Tulifanikiwa kumkamata mwanamume huyo baada ya kupata taarifa
kutoka kwa wasamaria wema,” alisema Rita.
Alisema siku ya Mwaka Mpya, alichukuliwa na dada yake na kumpeleka kwa mume wake huyo ili aanze maisha ya ndoa.
Hata hivyo, alisema alipofika, usiku huo walilala
kitanda kimoja wote watatu (baba muoaji, muolewaji na dada wa muolewaji)
na kwamba mwanamume huyo alianza kufanya mapenzi na dada yake na
baadaye akamgeukia ‘mkewe’ kuanza kumnyonya maziwa.
“Tulilala wote watatu na alifanya mapenzi na dada yangu, mimi akininyonya maziwa,”MWANANCHI