Bukobawadau

JE WAJUA? VYANZO VYA MAHUSIANO YA WENGI KUVUNJIKA

Sababu za kundi la pili ;Hisia za maumivu na machungu
Sababu kundi la pili ni yale matatizo ya kila siku ambayo wanandoa husuguana nayo baina yao. Matatizo haya mengine ni tabia za mtu alizokuja nazo ndani ya mahusiano yenu na anaziendeleza, na mengine yameibuka mkiwa tayari kwenye mahusiano (aidha unajua chanzo chake au hukijui). Matatizo au sababu hizi zaweza kusababisha mtengane, lakini huchukuwa uzito zaidi pale zinapochanganyika na zile za kundi la kwanza. Sababu hizi ni kama vile;
• Hasira kali
• Hisia za maumivu na machungu
• Wivu
• Tabia za kuhodhi (kila kitu wataka kiwe chako, kila kitu wajua wewe, kila kitu chakuhusu wewe)
• Tabia za kuwa mpingaji wa kila kitu (criticism)
• Kuwa na hisia zinazoyumba (mara furaha, gafla vijihasira)(mood swing)
• Kukwepa kuzungumza mambo yanayo wahusu
• Kukosekana kwa uaminifu (unfaithfulness)
• Kutopenda kuwa nyumbani mara kwa mara
• Kutofautiana kwenye matumizi ya pesa

Katika sababu zote hizi, wanandoa wengi waliokwisha kutalikiana wametaja ‘mapenzi nje ya ndoa’ kuwa sababu kubwa iliyowapelekwa kuamua kutengana.


Sababu za Kundi la kwanza (Hasira kali )

Kuwa na hasira sio kitu cha ajabu, wengi wetu tunahasira. Hasira inayozungumzwa hapa ni ile ya haraka, (short temper) isiyomruhusu mtu kufikiria mantiki ya kitu anachokasirikia, na kuamua tu kuchukua maamuzi ambayo mara kwa mara ni ya uharibifu au kusababisha maumivu kwa mwili au hisia za mwingine. Mara nyingi watu wajinsi hii hukimbilia kuomba msamaha mara wakishapoa lakini msamaha huo hata pale unapotolewa hauwezi kufuta makovu yaliyozalishwa na hasira zile. Inakuwa ngumu kwa wapenzi kuendelea na mahusiano hasa pale ambapo hasira na matukio haya yanajirudia mara kwa mara. Hata kama mpenzi mmoja ni mwingi wa rehema sana anajikuta anafikia ukomo wa uvumilivu. Tatizo lingine la tabia hizi ni kwamba, mara nyingi kila zinapotokea kupunguza kiwango cha penzi na imani kwa mwingine na taratibu unajisikia kumhofia mwenzako zaidi ya kumheshimu na kumpenda. Mbaya zaidi ukute mtu anatabia hizi halafu anatumia kilevi.


ITAENDELEA JUMAPILI.
Next Post Previous Post
Bukobawadau