Bukobawadau

MGOMO WA MADEREVA WA MALORI HUKO NZEGA LEO KUFUATIA MAUAJI YALIOTOKEA ALFAJIRI YA LEO JAN 26,2014

Huko Nzega hali ni tete baada ya  madereva wa Malori kugoma kufuatia tukio la majambazi kufanya unyama wa kumtoboa macho dereva na kumkata mguu tingo  alfajiri ya kuamkiaa leo Jan 26,2014.
Chanzo kinasema kuwa tukio hili limetokea  umbali wa km chache  kutoka mji wa Nzega  eneo la ZIBA   ambapo majambazi yaliteka malori matatu na kuwajeruhi madereva kwa kuwakatakata mapanga na kuwapora baadhi ya abiria, kufuatia tukio hilo madereva hao inasemekana walitoa taarifa polisi wakiomba  msaada lakini polisi walichelewa kufika eneo la tukio hali iliyosababisha majambazi hao kutokomea kusikojulikana.
 Kitendo kilichopelekea madereva ya malori zaidi ya 30  kufunga barabara hiyo kwa madai ya kumtaka mkuu wa mkoa wa Tabora afike ili waweze kumuelezea tatizo hili lipate ufumbuzi wa kudumu kwani limekuwa janga la mara kwa mara bila ya kuchukuliwa hatua .
Kutokana malori hayo kufunga barabara magari ya abiria na yale ya watu binafsi ikiwepo na la Mdau Gulam Skandar Visram yameshindwa kupita kuendelea na safari hivyo yamesababisha msururu mrefu .
Mpaka tunaenda hewani taarifa zinasema mkuu wa wilaya Nzega ndo alikuwa amefika eneo la tukio.
CREDIT; MDAU GULAM SCANDAR VISRAM KWA PICHA HIZI
Next Post Previous Post
Bukobawadau