Bukobawadau

PONGEZI KWA FLAVIANA MATATA

Kwanza kabisa naanza kumpongeza mdogo wangu Flaviana kwa kazi nzuri anayofanya ya kusaidia jamii hasa kupitia mfuko wake wa Flaviana Matata Foundation wa kusaidia watoto ili waweze kuipenda shule zaidi.
 
Sasa nilikuwa naomba tena aongeze na jingine hasa nilikuwa namkumbusha kuikumbuka jamii ya kabira ya Wanyambo wanaopatakana mkoa wa kagera wilaya ya karagwe na Kyerwa kama sikosei ndilo kabila lake. kumekuwa na tabia ya kukatishwa masomo watoto wa kike hasa wanaosoma sekondari, kwa kweli hilo ni tatizo sugu ndani ya wilaya zetu. 
Kwa sababu amesema tumuunge mkono naomba na hilo aliweke kwenye program yake ilii mfuko wake uweze kulifanyia kazi. watoto wa kike wamekuwa wakikatishwa masomo kwa kubebwa kwa lazima (yaani mtu anaoa kwa lazima ) naomba kupitia mfuko wako tulipige vita ni tabia ambayo imeishapitwa na wakati. 
 
Mdau Elewa .
Next Post Previous Post
Bukobawadau