Bukobawadau

KIJIJINI MUGONGO RUZINGA NI SHUGHULI YA MAZISHI YA MAREHEMU AURELIA NYAKATO RUGANGILA JIONI YA LEO JAN 21,2014

 Mchungaji akiongoza   Ibada ya Mazishi ya Marehemu Aurelia Rugangila aliyefariki tarehe tarehe 18 .1.2014  majira ya saa mbili usiku nyumbani kwake hapa kijijini Mugongo kata Ruhunga tarafa ya Kiziba wilayani Missenyi akiwa na umri wa miaka 92 ya kuishi.
Mwili wa Marehemu  Aurelia Rugangila aliye zaliwa 1922 na kafariki tarehe 18.1.2014 ukitolewa ndani 

 Ibada ya Mazishi ya Marehemu Omwana Aurelia Nyakato  Rugangila.
Taswira katika shughuli ya Ibada.
 Pichani ni wadau walioshiriki katika shughuli ya mazishi ya Marehemu Omwana Auleria Nyakato Rugangila aliyepata ubatizo mwaka 1930 katika kanisa la LUTHERAN Ruzinga.
Marehemu alipata elimu mpaka darasa la nne katika shule ya msingi Ruzinga .
 Mwendeshaji wa Shughuli hii Ndg Moses akitoa utaratibu  juu ya kinacho endelea na kinachofuata.
 Msiba huo ni mkubwa katika familia ya marehemu pia  ni mkubwa kijijini hapa, wasifu wa Marehemu ni mzuri na alipenda watu sana
 Mzee Alkadi Kataruga na Mama Kataruga pichani
Picha nyingine 100 za taswira ya shughuli hii zipo tayari katika ukurasa wetu wa facebook
Mzee Deus pichani kulia na Dada Mdogo wa Marehemu.
Heshima ya mwisho kwa marehemu Omwana Aurelia  Nyakato Rugangila aliyepatwa na mauti baada ya kuugua maradhi ya tumbo na shinikizo la damu zaidi ya miaka 10.
 Wadau wakapata fursa ya kuweza kuaga mwili wa Marehemu Bi Aurelia Nyakato Rugangila.
 Shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Bi Aurelia zikiendelea.
 Ndugu wa Marehemu Bi Aurelia Nyakato Rugangila katika zoezi la kutoa heshima za mwisho
 Kijana Nelly , ambaye ni mjukuu wa Marehemu Bi Aurelia Rugangila katika kuaga
 Shughuli ya mazishi ikiendelea leo jumanne  Jan 21,2014.
 Mazishi yakiendelea  kwa nyimbo na mapambio ya kihaya kama utakavyo ona  hapo badae kupitia account ya 'YOU TUBE'.
 Katikati ni Mdau  Thomas Charse Katikilo.
 Umati wa watu ukishiriki katika shughuli hii ya mazishi ya Marehemu Omwana Aurelia Rugangila.
Jeneza likiingizwa kaburini.
Mzee Deus akiweka udongo Kaburini.
Watoto wa Marehemu Omwana Aurelia Nyakato Rugangila wakiwekea udongo Kaburini
 Mjukuu wa Marehemu Omwana Aurelia Rugangila,Dr. Verus Kataruga akiweka udongo kaburini.
Mdau akishiriki kuweka udongo kaburini
Dr. Verus Kataruga baada ya kuweka udongo kaburini.
Pembezoni ni sehemu ya wadau walioshiriki mazishi haya, jioni ya leo Jan 21,2014. 

Shughuli ya mazishi ikiendelea.
Mdau Ben Kataruga katika mazishi ya Marehemu Bibi yake, kulia ni ndg Abdulrahym Kabyemela.
 Baada ya kuweka udongo kaburini ,Kitendo kinachofuata ni kusimika Msalaba kwenye Kaburi
Mchungaji akisimika Msalaba Kwenye Kaburi la Marehemu Bi Aurelia Rugangila.
 Wanafamilia wakiweka maua kaburini kwa pamoja
Ukoo wa Marehemu umewakilishwa na Mzee Deus katika zoezi la kuweka mashada Kaburini.
Akisukubwa kwenye kibaiskeli, Dada Mdogo wa Marehemu ,kuweka shada la maua kaburini.
 Zoezi la kuweka mashada ya maua likiendelea kama anavyo onekana Mzee Wilson pichani
Mama Kataruga akiweka shada la Maua.
Shughuli ya kuweka mashada ya maua katika kaburini imewahusisha wanaukoo,wakwe wa marehemu,watoto,wajomba,wajukuu,shemeji wa marehemu,viongozi wa dini na viongozi wa kijiji.
Mmoja kati ya viongozi wa Kijiji akiweka shada la maua kaburini.
 Zoezi la kuweka mashada likiwa linaendelea..
Baada ya zoezi la kuweka mashada kaburini , ni zamu ya wajukuu kuweka mishumaa.
Mdau Moses akiweka Mshumaa kaburini.
Wajuku wa Marehemu  Omwana Aurelia Nyakato Rugangila katika picha ya kumbukumbu.
 Nyumba ya Milele ya Marehemu  OMwana Aurelia Nyakato Rugangila 92
 Dr. Verus Kataruga , akitoa historia fupi ya Marehemu Omwana Aurelia Nyakato Rugangila.
Kushoto ni Ndg Kamuzora ,akifanya yale ya kisasa, katikati ni  Ndg Cathbert Basibila.
Mzee Deus akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia ya Marehemu Bi Aurelia.
 Kutoka kushoto ni Ndg Kamuzora, Ndg Kathbert Basibila,Blogger Mc Baraka wa mwisho ni Omulangira Ben Kataruga.
 Mdau Ruge akicheck na mdau wa Kijijini  Mugongo ndani ya kata ya Ruhunga.
Mwisho anaonekana Mdau akichukua zake  kasi.
Kwa masikitiko makubwa Bukobawadau Blog tunatoa pole kwa ndugu na jamaa wa Marehemu Omwana Aurelia Nyakato Rugangila,Msiba huo ni mkubwa katika familia yenu tunamuomba  Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema poponi Ameen!!!

Next Post Previous Post
Bukobawadau